Uzee dawa: Msikilize Jenerali Ulimwengu

Nimeamini kuwa uzee ni dawa na kuishi kwingi ni kuona mengi.

Msikilizeni huyu mzee wetu alafu lazima utajifunza kitu cha kukusaidia maishani mwako.

Kuna haja huko tunakoelekea kuwa na jitihada za makusudi kuwahimiza au pengine kuhamasisha watu kusoma katiba inayokuwepo kwa wakati huo na kuielewa kusudi tunapokuwa na viongozi walioteuliwa au waliochaguliwa wasiende kuwa court jesters. Hii ni pamoja na elimu ya uraia ili kuondoa aibu ya watu kujitoa ufahamu kwa kujidhalilisha mbele ya uma kwa kuzungumza unexpected words kama " umenitoa majalalani"
 
Haya sawa Kanyawela
 
Yule kalamaganda kabugi hajitambui ndiyo maana aliamua kujidhalilisha kisa kumfurahisha mteuzi wake.
 
Nikiwasoma wengine humu ndani naona ni maji yaliyokwisha mwagika. Matumaini yangu ni kwamba kama mna watoto au mna mpango wa kuwa nao, mtakuwa na ufahamu wa kulea wakue na mtazamo wa kimaisha wa Jenerali na sio Profesa
 
Yule kalamaganda kabugi hajitambui ndiyo maana aliamua kujidhalilisha kisa kumfurahisha mteuzi wake.
Kuna kitu najiuliza sipati jibu. Wengi wakiwa kwenye nafasi za taaluma zao wanaonekana ni ma genius. Lakini wakiingia kwenye nafasi za kisiasa wanakuwa watu tofauti sijui ni kitu gani kinawasibu! Nisaidieni hapo!
 
Kuna kitu najiuliza sipati jibu. Wengi wakiwa kwenye nafasi za taaluma zao wanaonekana ni ma genius. Lakini wakiingia kwenye nafasi za kisiasa wanakuwa watu tofauti sijui ni kitu gani kinawasibu! Nisaidieni hapo!
Kwa mujibu wa uchunguzi ni kwamba unapo jiunga na ccm basi weledi wako unaukabidhi mapokezi.
 
Kwa mujibu wa uchunguzi ni kwamba unapo jiunga na ccm basi weledi wako unaukabidhi mapokezi.
Niliwahi kuambiwa pia kuwa miaka ya nyuma ( sijui kama hadi sasa bado inaendelea) makuruta wa chuo cha Polisi siku ya kuripoti chuoni huko Moshi, wakifika getini kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani kila mmoja alikuwa anaambiwa kuchimba kishimo kidogo na kuambiwa kuwa akili zao zote za kisomi waziweke humo na kuzifukia. Na kwamba akili zitakazokuwa zinatumika pale ni za maafande. Siku wakimaliza mafunzo ndipo watachukua akili zao walizokuwa wamezifukia na kuondoka nazo.
 
Aisee hiyo ni kali ya mwaka kama kweli ipo
 
Wape hao wa jalalani siyo mimi- standing tall and proud!
 
Huyu mzee ugali wake wa Gazeti la Raia Mwema ulitingishwa kidogo ndiyo maana anahaha. Wengi wanaoponda serikali ya awamu ya tano walikuwa wanafanya biashara za kanjanja kanjanja wakazinguliwa.
Sidhani kama unamfahamu vizuri huyo dingi.ajaanza kua serious na mambo ya msingi leo.na ni mzee wa nyeupe nyeupe nyeusi nyeusi.
 
Nadhani wengi walisahau kuchimbua akili zao baada ya mafunzo ndio maana nchi mwendo ki afande afande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…