JoJiPoJi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2009
- 2,935
- 3,346
Mkuu ni wk ya pili hii inaenda baada ya shipper kusubmit manifest corrector. Siku zinakatika tu, kila siku mara system iko down. Mara oh mzigo wako ulikwishatoka kwenye system wakati si kweli na upuuzi mwingine kibao. .
Mkuu Bobby Mimi Sijaona kosa la TPA na TRA kwenye issue yako.
Utaratibu upo hivi, Shipping Line anajukumu la kutuma manifest TRA, na Discharge list TPA, itakapotokea tofauti kati ya chassis namba iliyopo kwenye gari na iliyotumwa kutoka shipping maana yake ni Kuwa hautaweza kutoa hiyo gari.
Inapotokea hali kama hiyo consignee anatakiwa arudi kwa shipper ili watume correction notice kwa shipping line.
Shipping Line akishapata correction notice anafanya amendment ya details zako kwenye system ya TRA, hawa wanatakiwa wa approve ili uweze kuendelea na taratibu za kutoa gari yako.
Sasa ikitokea labda meli iliyobeba gari yako ilipangwa bandari kavu, kidogo lazima utachelewa na hii inatokana na amendment zinapofanyika TPA wanapata ugumu katika kuandaa movement sheet.
Kwa hatua hizi nilizojaribu kuelezea Sijaona uzembe unaosemwa wa TRA na TPA.
Bado nataka kukusaidia, LINE GANI ULITUMIA KUSAFIRISHIA MZIGO WAKO?