Uzembe wa Askari kulenga shabaha na kupoteza risasi 49 unaposingiziwa ushirikina

Halafu kuna yule mama alisema askari "wao" hawawezi kupiga risasi 16 na kukosa kwenye kampeni😂😂

Sijui jina lake anaitwa nani yule mama. I'll nashangaa wamama wanapingana kauli zao
Nazani utakuwa una mzungumzia yule dikiteta mwenye jinsia ya kike
 
Nilipoiona hii taarifa jana nilijua kunawapumvavu watakuja na mawazo kama haya.

Kumbe kweli bwana si huyu hapa hahahaaaa!!!!
 
Isiyokuwasha hujailamba. Hujajua nini kilitokea mpaka zikatumika risasi zote hizo. Tungesikia story kutoka ka Askari na mashuhuda ndipo tungeweza kusema neno.
Sawa lakini lisihusishwe na masuala ya kishirikina.

Pia vyovyote ilivyo hakuna Askari Pori(well trained Ranger) utamwambia umetumia risasi 49 kumlenga Fisi ukamkosa akakuona Mtu unayejitambua...atakuona unadhalilisha tu taaluma za Watu.
 
Niliwahi kusikia risasi moja mpaka kufika store ya jeshi, inagharimu 150k za kitanzania. Sina uhakika, na siwezi kuthibitisha!
Huenda ila mimi si mjuzi wa eneo hilo...na sijui zilitumika zile za Wanyama au hizi hizi za kawaida.
 
Habari zinasema kuwa fisi huyo alikuwa 'mahiri' wa kukwepa risasi, kama huu ni ukweli (alikuwa anakwepa wakati anapigwa), basi kuna uwezekano wa kumaliza risasi nyingi kabla ya risasi moja kumpata.

Wanasema fisi huyo ni wa ushirikina, sasa kama unasema kutumia risasi zote hizo ni uzembe, basi unatakiwa useme kuwa duniani hakuna kitu kama hicho (ushirikina). Humu kuna mtu mmoja anaitwa mshana junior, tumuulize, anaweza akawa na majibu mazuri juu ya tukio hili.
 
Hio ni true kabisa huyo fisi katokea milima ya izimbili ni wa ukoo wa mwanamalundi na isike namfahamu sana saiv yupo huku katabi katavi mizimuni kwa wanaoifahamu Tabora hilo ni Jambo la kawaida sana ni kweli walimkosa risasi zote 49 na huwa anatumika sana kumalizia kizazi pinzani cha machief
 
Tuna taifa lenye ujinga sana.

Na wenye akili wanajua ku take advantage....ndio yale ya kuambiwa Pesa za Vikoba zimebenwa na chuma ulete.

Taifa linahitaji tiba hili...taifa limejaa ujinga.
 
wewe ni mbumbumbu sana na hauijui dunia. kalaga baho.
Kwa upuuzi kama wako tutaendelea kuwaona Wazungu kama Miungu watu.

Tunahitaji kuwa na Watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi, hao Wenzetu hawana miujiza ni bidii tu na kuachana na akili za kijinga.
 
Asante sana[emoji736][emoji817][emoji1534][emoji1548]
 
Sasa kama wana intelijensia kwamba risasi hazifanyi kazi kwanini waendelee kutumia hizo risasi ? Kuna mambo ukishayakubali nusu tu ni kwamba unaingia kwenye unkown territory yaani itabidi kila kitu umeze tu (hakuna haja ya logic wala kuuliza) na tungeendelea hivyo tokea kali mpaka leo watu wangekuwa wanatolewa kafara na kuzikwa na wafalme wakiwa hai....

Haya mambo yafanyike individually huko ila sio kwenye taasisi muhimu wala kuyafanya kama taifa...
 
Mashuhuda na askari wamesema fisi alikuwa anakwepa risasi! Wewe uliona wapi mnyama anayekwepa risasi? Kwa mtu mwenye utaalam kidogo tu na mambo ya bunduki na risasi atakucheka sana akisikia unasema eti fisi anaweza kukwepa risasi.
Wanashindwa kutofautisha uwezo wa kulenga shabaha na Fisi kukwepa.

Ni kwa kuwa kila aliyekuwepo pale alikuwa na mawazo ya kishirikina...lakini tafsiri sahihi ule ni uzembe na uwezo mdogo wa Askari.
 
unafiki ni kitu kibaya sana, ina maana hujui kama ushirikina upo?
Hakuna ushirikina, ni imani zinazopandikizwa kwa watu wasiotaka kutumia akili.

Mtu akiugua sasa ili kutokuwajibika kujua tatizo lililomsibu ni nini basi mnaishia kuambiana tu kalogwa.

Wenzenu huko wanaingia maabara, wanakesha mpaka wanagundua kuwa Mwili umeingia vijidudu na aliyeviingiza mwilini ni Mbu, na baadae wanatafuta na namna ya kuwatoa/waangamiza vijidudu na Mtu unapona.

Nyie mmebung'aa tu kama mawe mkisubiri mletewe chloroquine mmeze.
 
Acha kukuza mambo hapo Congo ukinunua AKA 47 unapewa na ndoo ya risasi. Tatizo linakuja askari wetu hawana ata shooting range ambazo zinakeep their skills walizonazo kwenye shabaha wakipata fursa inabidi watumie kikamilifu kama hivo.
 
Duh, kama nchi bado tuna safari ndefu sana.
 

Story za kusadikika zinazoaminiwa na wajinga. Hakuna uchawi/ushirikina/nguvu za giza.

NB: ujinga sio tusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…