DOKEZO Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA

DOKEZO Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Snapinsta.app_450052187_18063941032570666_8514048800260325639_n_1080.jpg

Juzi usiku tulimpeleka hospitali ya Nanguji mwanachuo mwenzetu ambae alizidiwa, wakamfanyia vipimo na kusema utumbo umejikunja hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kwa haraka, kwa pale gharama zilikuwa ni laki 8 hivyo tukaombwa kupelekwa hospitali ya mkoa kwasababu ya unafuu wa matibabu, tukapewa ambulance ikatupeleka hadi Hospitali Kuu ya mkoa Morogoro, pia tukawasiliana na mama wa mwenzetu nae akaanza safari ya kuja.

Baada ya kufika pale na jinsi situation ilivyokuwa ya dharura lakini tuliambiwa Daktari wa upasuaji hayupo available kwa muda huo kwasababu anahudumia wagonjwa wengine, tulisubiri pale mpaka asubuhi ilipofika na mama wa mwenzetu pia akawa ameshafika, still situation ya kumkosa Daktari ikaendelea, uzuri mama wa mtoto alikua ni Daktari pia hivyo baada ya kuangalia vipimo alivyokuja navyo mwanae kutoka hospitali ya Nanguji vilikuwa very clear kwamba hii ni emergency situation inayopaswa ishughulikiwe kwa haraka zaidi, wao wakazidi kusema Daktari wa upasuaji hayupo available.

Mama wa mwenzetu akaomba apewe room afanye upasuaji mwenyewe, niliondoka nilipoona wanampa vifaa kweli, na hiyo ilikuwa inaelekea jioni sasa, usiku nikampigia yule mama akasema hawakumruhusu na wamemwahidi kesho yake ndio atafanyiwa upasuaji.

Basi nikalala kwa amani nikijua asubuhi mwenzetu atapata huduma, lakini asubuhi nikafika hospitali na kukuta Mgonjwa bado hajapatiwa matibabu, nilikuwa na uji na chakula wakasema hawatapokea nirudi navyo nyumbani, nikapokea simu kwamba ndugu yetu, rafiki yetu ameaga dunia.

Kwakweli jambo hili limeniliza sana na nimeshindwa nikalia kimya.

Amefariki tarehe 4/Jul/ 2024 yaan leo.

Siku mbili zote mwenzetu anaishi kwa mateso mpaka umauti wake unamkuta, alikuwa bado wiki moja afanye final exams katika chuo cha SUA na alikuwa mwaka wake wa mwisho, kwakweli imeniuma naomba mpige sauti juu ya hili na uchunguzi ufanyike juu ya kilichotokea.

8e1048a6d72141549a9902c921d31d7b.jpg

MAJIBU YA MGANGA MKUU WA MKOA
JamiiForums imewasiliana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Urio Kusirye amejibu hivi:

Sijasikia popote kuhusu hilo suala, kama wahusika wanahitaji taarifa waje ofisini tutatoa taarifa, hatuwezi kutoa taarifa Mitandaoni.

Kama wahusika wapo waje tutawapa taarifa kisha wao wakitaka watazitoa Mitandaoni tutawaruhusu, sio sahihi kutoa taarifa mitandaoni hata kama amekufa. Wakija tutatoa ushirikiano kwa Asilimia 100.
 
Inauma sana, mama mzazi kwa kushuhudia kifo cha mwanaye kutokana na uzembe wa hospitali itakabaki kuwa kumbukumbu mbaya kwake.
Kwanza pole kwa familia. Kuna watu hawataona uhusiano wa CCM na serikali yake na hili tukio lakini ukweli ni kuwa vina uhusiano. Tunarudi pale pale, utasema mimi sihusiki na siasa lakini madhara ya uongozi mbovu yanatupata wote.
 
Hayo ndio maisha ya watu wa tabaka la chini kila siku lakini nani anajali maana hata victims wenyewe huamini "ndio ashakufa kama ahadi ya Mungu, kifo hakizuiliki"..

Na wengine wakisikia wizara ya afya inalalamikiwa, si ajabu wakaitetea kwa sababu tu alietoa maneno ni mange au mwanaharakati yoyote. Mbaya zaidi, watu huwa tunashtuka pale tu linapotufikia directly Ila kama halituhusu tunakaa kimya, hii ndio system
 
Ni kweli mkuu lakini kwa issue ya emergency, labda ithibitike kulikuwa na wagonjwa wenye serious case kumzidi.
Ngoja wachunguze unaweza kusikia madaktari wengine wapo likizo ....Hii ndio bongo na daktari anataka muda wa kupumzika
 
Usimlaumu Dr Wala Hospital unaweza Kuta hilo tatizo ni la CCM na serikali Yao,

watumishi wa afya hawatoshi watu wanakuwa overworked kama punda ukute Dr muhusika ameunganisha shift siku 3 mfululizo bila kupumzika akaona akapamzike zake asije akafia kazini.
 
Km mama wa mgonjwa ni Dr, na aliomba vifaa afanye upasuaji mwenyewe, kwann walimkatalia? Dr wa hospital si yuko na majukumu mengine, sasa kwann wamkatalie Dr ambaye yuko available kufanya huo upasuaji?

Inauma sana [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Tusikilize na upande wa Pili.. nashauri Moderator tafuteni usahihi, au kuwasililiza upande wa pili.. maana habari imeandikwa kishakibi sana . kama ni emergency kwa sheria za nchi yetu angefanyiwa kule kule kwa laki nane....
nadhani kulikuwa na sitofahamu ... pengine madaktari walisha ona hakukuwa na uwezekano wa kupona hata wangefanya hiyo operation..
 
Back
Top Bottom