Juzi usiku tulimpeleka hospitali ya Nanguji mwanachuo mwenzetu ambae alizidiwa, wakamfanyia vipimo na kusema utumbo umejikunja hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kwa haraka, kwa pale gharama zilikuwa ni laki 8 hivyo tukaombwa kupelekwa hospitali ya mkoa kwasababu ya unafuu wa matibabu, tukapewa ambulance ikatupeleka hadi Hospitali Kuu ya mkoa Morogoro, pia tukawasiliana na mama wa mwenzetu nae akaanza safari ya kuja.
Baada ya kufika pale na jinsi situation ilivyokuwa ya dharura lakini tuliambiwa Daktari wa upasuaji hayupo available kwa muda huo kwasababu anahudumia wagonjwa wengine, tulisubiri pale mpaka asubuhi ilipofika na mama wa mwenzetu pia akawa ameshafika, still situation ya kumkosa Daktari ikaendelea, uzuri mama wa mtoto alikua ni Daktari pia hivyo baada ya kuangalia vipimo alivyokuja navyo mwanae kutoka hospitali ya Nanguji vilikuwa very clear kwamba hii ni emergency situation inayopaswa ishughulikiwe kwa haraka zaidi, wao wakazidi kusema Daktari wa upasuaji hayupo available.
Mama wa mwenzetu akaomba apewe room afanye upasuaji mwenyewe, niliondoka nilipoona wanampa vifaa kweli, na hiyo ilikuwa inaelekea jioni sasa, usiku nikampigia yule mama akasema hawakumruhusu na wamemwahidi kesho yake ndio atafanyiwa upasuaji.
Basi nikalala kwa amani nikijua asubuhi mwenzetu atapata huduma, lakini asubuhi nikapokea simu kwamba ndugu yetu, rafiki yetu ameaga dunia.
Kwakweli jambo hili limeniliza sana na nimeshindwa nikalia kimya.
Amefariki tarehe 4/Jul/ 2024 yaan leo.
Siku mbili zote mwenzetu anaishi kwa mateso mpaka umauti wake unamkuta, alikuwa bado wiki moja afanye final exams katika chuo cha SUA na alikuwa mwaka wake wa mwisho, kwakweli imeniuma naomba mpige sauti juu ya hili.