DOKEZO Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA

DOKEZO Uzembe wa Hospitali Kuu ya Mkoa Morogoro umesababisha kifo cha Mwanafunzi wa SUA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Si rahisi kihivyo,angekufa wakati anafanyowa upasuaji namama yake ingekuwa msala
Ila kufa bila kupatiwa huduma na yupo hospitali kwa siku mbili sio msala?

Linapokuja jambo la kuokoa maidha ni bora kufanya kuliko kutofanya kabisa.
 
Mimi sio Dr ila naomba nikuulize. Utumbo kujikunja ndio intestinal obstruction au intestinal volvulus( which is medical emergency)?
Humu jeifu kila mtu si huwa tu anajiandikia, jamaa ukute katoka zake google akaja kuleta critics humu, haha
 
Wakuu kifo cha huyo mwanafunzi kimeniuma sana japo hata simfahamu sababu hilo tatizo limeshanikuta.

kilichonifanya niumie zaidi ni maumivu aliyoyapata sababu nayajua nilishayapitia.

Baada ya operation kulazwa siku tano na kuruhusiwa nikasoma discharge form imeandikwa......
A patient suffered from "intestinal obstruction secondary to sigmoid volvulus'' He is doing better, passing slool and He is discharged.

Yaani tatizo langu ilikuwa ni zaidi ya intestinal obstruction(utumbo kujikunja) iyo secondary to sigmoid volvulus (yaani baada ya kujikunja na kuziba, tatizo lika develope utumbo ukavimba mvimbo mkubwa sana)

Madaktari walishangaa wanashangaa imekuwaje nikaweza kuishi na hilo tatizo mpaka lika develope kiasi hicho kumbe bana kilichokuwa kinanisaidia kila siku alfajiri nilikuwa nakimbia cross-country ndo chakula kitapita kwa tabu kwenye iyo brokadge, ndo maana ilikuwa kukata gogo ni mpaka nitoke running.

Siku ya kuugua kila kitu nachokula kina rudi chochote hata maji natapika, nasikia mpwito nikienda toi sikati gogo narudi ndani tumbo linauma kinyama siwezi kutembea wima nimenyooka, urefu wangu ni futi 6 na nchi 3 takini nilikuwa natembea kimo cha futi 3 kupunguza maumivu.


kufupisha nilienda hospitali usiku saa nane, kelele nilizokuwa napiga yaani kila mtu ile hospitali alijua hapo tatizo bado halijajulikana nimepigwa drip tu nasikia maumivu kinyama.

pakakucha maumivu ni makali nikaambia nesi maumivu nayosikia ni makali sana, hee nesi anasema dirisha la dawa bado kufunguliwa nisubili wafungue (hapo nilikuwa na bima ya NHIF) ikabidi dawa ya maumivu ikanunuliwe mtaani ikaletwa nesi akanichoma sindano.

ile sindano sikuisikia wakati anachoma, nikamiuliza tayari ushachoma akasema eeeh maajabu ile sindano ya kutuliza maumivu haikusaidia chochote maumivu ndo yakaongezeka mpaka saa tatu ndo kupelekwa utra sound ndo tatizo kujulikama hapo napiga mwano kinyama.

kule utra sound aliyekuwa ananifanyia examination kwa sababu nimelala sioni kwenye monitor nikamuuliza shida ni nini? akawa anajidai hii mashine mbovu yaani hata haionyeshi vizuri, nikamuambia nilisoma psychology chuo najua unachokifanya wewe nambie tu shida nini mimi naweza ku handle taarifa yoyote lakini hakunambia.

nikarudi wodini nikaambiwa natakiwa nifanyiwe emergency operation, nesi akaja kuniandaa nisaini operation ifanyike, sikuwa na weza ku saini alisaini girlfriend wangu, huyu ndo alienipeleka hospitali baada ya kuona hali yangu sio nzuri kulala geto mwenyewe nilimpigia simu jana yake nilikuwa nae gheto.

nikaandaliwa ule mpira wa mkojo unapitishwa kwenye mashine na nesi mrembo(ila hamfikii shemeji yenu) nmejikaza muda huo sipigi kelele naambiwa pole utapona, kamaliza anasukuma kitanda kwenda theater kuna ka umbali nikashindwa kuvumilia maumivu nilipiga kelele nazani hakuna mtu kwenye ile hospitali aliyewahi kupiga kelele kubwa vile yaani wanaojifungua walikiwa wananiulizia hizo kelele zinatoka wapi?

kule theater nikawekwa kwenye kitanda, nikaunganishwa nyaya nyaya zile, akapachika sindano kwenye kile kidude cha drip nilikiwa nacho mkononi nikalazwa chali pozi nimetanua mikono.

nikamuambia yule jamaa hilo pozi naumia nigeuke akaniruhusu, hapo bado wawengine wanavaa Sergio anasubiriwa, maama ilikuwa emergency halafu ilikuwa jumatano sio siku ya operation maama ile hospitali ni ya wilaya na tu, Operations zote huwa wana zi schedule juma nne na alhamis.

Eeh wana chelewa kuja maumivu makali hapo kile ki sindano sijui cha nini kipo kwenye mkono, yule mwamba alokiweka na yeye yupo. kichwa nikafikiria hiki ki sindano ni cha kunizima nikapata wazo nikipushi nizime maana maumivu ni makali sana, yaani muda huo nilikuwa natamani hata nife,

ite natala kupush dawa yule mwamba aliniona alifoka UNATAKA KUFANYA NINI UTAKUFA halafu akaniweka lile pozi chali bila kujali maumivu ya lile pozi sikujua kilichoendelea tena baada ya masaa mawili na nusu ndo natoka theater.

yale maumivu ya usiku niliongea na maza girlfriend akawa anampa updates, kipindi naenda theater maza akafunga safari kutoka mkoa mwingine maama mimi niko kikazi mkoa mwingine. natoka theater akapewa updates.

nimekuja kushtuka usiku bi mkubwa kashafika, wafanya kazi wenzangu ofisini wapo hawaamini maana jana yake siku niliyoanza kuumwa nilikwepo kazini.

Keshoyake Dr anapita swali ya kwanza kuulizwa "umejampa" nikamwambia ndio akanamia safi hiyo ni hatua nzuri ndo kujua kumbe kujampa ni suala la msingi sana, akanambia unaweza kutembea nikamuambia ndio bas nika natembea mule room napita kwenye korido ila natembea kizombi kuna mtu pembeni yuko standby kunidaka.

Dr alikuja kutoa lile bandage hee kuona mshono mrefu na hivi mimi ni mrefu yaani tumbo lote vertical umeshonwa nyuzi 27, nikawa naogopa kutembea nahisi mshono utafumoka utumbo umwagike kumbe ni kutu ambacho hakiwezekani.

kuruhusiwa nikaenda geto kuuguza mshono hapo, hapo huduma zote kupikiwa chakula, kupelekwa haja ndogo na kubwa, kusafishwa, kubadilishwa nguo kila kitu anafanya yule girlfriend wangu, maza hana kazi alivoona naendelea vizuri na huduma zote napata akanambia hata akiondoka nikamuambia poa akasepa kuendelea na majukumu yake.

Kabla hajaondoka maza alinambia huyu mwanamke wako usimuache nikamuuliza kwa nini hata hakunambia chochote, bas bana niliuguzwa huku nikiwa comfortable nakiri sidhani kama ningekuwa comfortable kama ningeuguzwa na mtu yoyoye mwingine, vuta picha unataka kwenda kukata gogo upekekwe ushikiliwe kwenye kukaa huko chooni umalize umwagiwe maji kujisafisha ufutwe majimaji uvalishwe urudishwe ndani.

Hizo kazi ni mara 100 azifanye mwanamke wako utakiwa comfortable kuliko azifanye mama yako. huwa nawashangaa kataa ndoa hawafikirii siku wakiugua,

Girlfriend wangu kabla ya mimi kuugua nilikuwa nimesha mpaga assignment kibao(bila yeye kujua) za kuwa mke alikuwaga amesha pass hizo assignment sema bado nilikuwa sijatangaza kumuoa. akanipa bonus ambayo sikumuambia maana aliachq kazi alikokuwa anafanya ili aniuguze saivi ni mke wangu halali na tuna watoto.

Kuhusu kutuliza mshono, nilikuwaga sielewi maana yake nilikuwa najua ni msemo tu wa kumwambia mtu atulie, nikajua baada ya kuupata mshono yaani inatakiwa uutulize tena usiwe na haraka utembee kizombi hashwaaa maana ukiutikisa mshono ni hatari,

kuna siku naenda hospita waangalie maendeleo wa mshono, chombo nimepanda dereva akapita kwenye vile vituta vidogovidogo kwa speed grrrriiiiii ebanae ndo nikaelewa maana ya kutuliza mshono.

Samahani kwa hili bandiko refu nimejikuta tu naandika nimemuhurumia sana huyo kijana maumivu aloyapata sababu I felt the same pain.
Hahah pole sana mkuu na tuliza mshono.
 
Kama kulikua na upungufu wa madaktari wangewaeleza ukweli na wangeona cha kufanya,Intestinal obstruction ni surgical emergency na inahitaji immediate surgical intervention siku 2 halafu mtu abaki haipo hiyo uzembe,uzembe,uzembe..rest in peace young academician
Huyo hakuwa na IO, acheni ujuaji bhn madaktari wa jeifu.
 
Halafu Dk mwenzao
Napata picha mwl mimi,ningeshushuliwa nijute
Hii ndo Tanzania
Kila mtu anashangaa mpk Rais
Ila kiukwelii tunahitaji Gen Z
Tanzania haihitaji Gen z inahitaji watu wenye awareness kubwa na wàtu waliotayari hao Genz kwani Tz hawapo ? Si wapo
 
Rushwa ni mbaya sana. Mtu unaweza kufa hivihivi kumbe mtaka rushwa anakuzungusha ili umpe hela na wewe huelewi kama anataka hela..
 
Siku mbili zote mwenzetu anaishi kwa mateso mpaka umauti wake unamkuta, alikuwa bado wiki moja afanye final exams

Sasa wadogo zanguuuu......

Kama mwenzetu amekufa kwa uzembe, kwa nini mnasema BWANA AMETOA BWANA AMETWAA ??????????

Masikini ya Mungu, elimu, utamaduni, vichwa, upeo, na ma imani ya sisi watu wa the third world!
 
Kwanza pole kwa familia. Kuna watu hawataona uhusiano wa CCM na serikali yake na hili tukio lakini ukweli ni kuwa vina uhusiano. Tunarudi pale pale, utasema mimi sihusiki na siasa lakini madhara ya uongozi mbovu yanatupata wote.
Ukiona mtu anasema hajihusishi na siasa jua ni kichaa...Siasa ndo maisha yetu imebeba maono na muelekeo kwenye utafutaji wetu na afya za wenzwtu nk.

Mwisho CCM itakuja kutoa rambi rambi kisha ikamsifia Rais ndo kitu wanachowez
 
Juzi usiku tulimpeleka hospitali ya Nanguji mwanachuo mwenzetu ambae alizidiwa, wakamfanyia vipimo na kusema utumbo umejikunja hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kwa haraka, kwa pale gharama zilikuwa ni laki 8 hivyo tukaombwa kupelekwa hospitali ya mkoa kwasababu ya unafuu wa matibabu, tukapewa ambulance ikatupeleka hadi Hospitali Kuu ya mkoa Morogoro, pia tukawasiliana na mama wa mwenzetu nae akaanza safari ya kuja.

Baada ya kufika pale na jinsi situation ilivyokuwa ya dharura lakini tuliambiwa Daktari wa upasuaji hayupo available kwa muda huo kwasababu anahudumia wagonjwa wengine, tulisubiri pale mpaka asubuhi ilipofika na mama wa mwenzetu pia akawa ameshafika, still situation ya kumkosa Daktari ikaendelea, uzuri mama wa mtoto alikua ni Daktari pia hivyo baada ya kuangalia vipimo alivyokuja navyo mwanae kutoka hospitali ya Nanguji vilikuwa very clear kwamba hii ni emergency situation inayopaswa ishughulikiwe kwa haraka zaidi, wao wakazidi kusema Daktari wa upasuaji hayupo available.

Mama wa mwenzetu akaomba apewe room afanye upasuaji mwenyewe, niliondoka nilipoona wanampa vifaa kweli, na hiyo ilikuwa inaelekea jioni sasa, usiku nikampigia yule mama akasema hawakumruhusu na wamemwahidi kesho yake ndio atafanyiwa upasuaji.

Basi nikalala kwa amani nikijua asubuhi mwenzetu atapata huduma, lakini asubuhi nikapokea simu kwamba ndugu yetu, rafiki yetu ameaga dunia.

Kwakweli jambo hili limeniliza sana na nimeshindwa nikalia kimya.

Amefariki tarehe 4/Jul/ 2024 yaan leo.

Siku mbili zote mwenzetu anaishi kwa mateso mpaka umauti wake unamkuta, alikuwa bado wiki moja afanye final exams katika chuo cha SUA na alikuwa mwaka wake wa mwisho, kwakweli imeniuma naomba mpige sauti juu ya hili.

Hili ni funzo kwa mama dakitari na madakitari wenzake kuwa malalamishi yetu kuhusu uzembe wa madakitari ni wa kweli.
 
Hii serikali ipo radhi kununua magari ya kumwagia maji washa upinzani kuliko kuajiri madaktari ambao wamejaa mitaani hawana ajira rasmi.
 
Ina uma sana pole kwa wote kwa msiba.
Tatizo ni mifumo labda Mungu alitaka kumuonesha huyo Daktari kwamba hii ajira ya kuhudumia watu ukiifanya vibaya kwa watu usio wajua pia ipo siku hata wewe yatakukuta.
Vijana wengi walipokuwa wanatafuta ajira wanakuwa wapole wakipata kazi wanatufanyia mambo ya ajabu na kusahau kwamba nao wana ndugu zao wanaoweza kukutana na kadhia kama hiyo kwa mfano mimi kila nikienda hospitali hawa jamaa wanavyokunyanyapaa utadhani wao na familia zao huwa hawaumwi, nikienda Polisi wanavyo nipokea kama vile kutafuta haki ni kosa na ni usumbufu kwao,nikienda Ardhi watumishi wao wamekaa mkao wa kuomba rushwa sijui tatizo ni nini? Mifumo yote hii ili ikae sawa kuna haja ya watu wa haki za binadamu wachukue likizo kidogo watuachie tu deal nao kwanza ala wakishika adabu warudi kutetea haki.
 
Mama yake hawezi kuumia maana inaonekana kuna shortage ya madaktari na aliyekuwepo alikuwa anawafanyia upasuaji mama wajawazito,dont be judgemental kazini,mjamzito ni first priority
Siku 2 anafanya caesarian sections.
 
Umasikini na uzembe = kifo


Laki nane , mgelipa tu cheap is expensive

Inaumiza sana
 
Inauma sana, mama mzazi kwa kushuhudia kifo cha mwanaye kutokana na uzembe wa hospitali itakabaki kuwa kumbukumbu mbaya kwake.
Hii fani ya udaktari imeingiliwa na watu wasiokuwa na wito, wasiofuata tena maadili ya hii huduma.
Inasikitisha..!
 
Tusikilize na upande wa Pili.. nashauri Moderator tafuteni usahihi, au kuwasililiza upande wa pili.. maana habari imeandikwa kishakibi sana . kama ni emergency kwa sheria za nchi yetu angefanyiwa kule kule kwa laki nane....
nadhani kulikuwa na sitofahamu ... pengine madaktari walisha ona hakukuwa na uwezekano wa kupona hata wangefanya hiyo operation..
natamani nikuone sura yako nijue kama inafanania na haya maandishi uliyoandika......
btw ni maoni yako pia sio dhambi kutoa maoni yako
 
Hivi ni moja kati ya madudu mengi yanatokea Afrika kwa sababu ya kuwa chini ya tawala zinazojali madaraka na sio uongozi...
 
Kwanza pole kwa familia. Kuna watu hawataona uhusiano wa CCM na serikali yake na hili tukio lakini ukweli ni kuwa vina uhusiano. Tunarudi pale pale, utasema mimi sihusiki na siasa lakini madhara ya uongozi mbovu yanatupata wote.
Umesema ukweli kabisa!
 
Back
Top Bottom