Ahsante Sana Mtoa Uzi huu,umefanya kile Muumba wako amekuwezesha kufanya Kwa ajili ya watu wengine na hii ndio inatakiwa!
Ila kiukweli wabongo tuache kubaniana,tuache choyo,huwezi kuwa mtu tajiri au mwenye mafanikio yenye furaha kama umezungukwa na kundi la masikini au watu wasio na ajira,mtoe mwenzio huwezi jua nawe utatolewa Kwa style gani,kwanza hakuna aliyefika juu bila kushikwa mkono.Bongo bila connection huwezi toka Uwe una vigezo au huna kama huna connection sio rahisi kutoka! Unaona hata viongozi wetu wakisha pata madaraka wanazilinda connection zisitoke nje ya watoto au watu wao na kuwaacha wengi hawana pa kushika.
Nije Kwa upande wa sisi pia wasaka ajira,hakikisha unakuwa apdated,chapa CV zako vizuri scan vyeti vyako vizuri weka mtandaoni,enzi za kuzunguka na bahasha zimeisha pitwa na wakati,like pages follow pages zinazo toa ajira mfano Kwa wale wenya ma CV makubwa ingia mtandao wa LinkedIn huko kazi Yao kubwa ni mambo hayo,fanya setting za kile ulichosomea utakuwa unapata notifications Kila aina ya kazi inaendana na wewe! Pia wale madogo wasomi wasomi miaka 19 Hadi 20 ,30 Kuna ki website kinaitwa Youthop wanatoa Sana ufadhiri wa madogo kwenda kusoma nk!
Na wewe ukifanikiwa acha kuwabania wenzio,toa connection Kwa watoto wa masikini acha roho mbaya! Watatubania TU ila siku Mungu Atatutoa TU na sisi.
Ma HR acheni roho mbaya! Wakuu wa ma NGOs wanakuja na mishahara kabisa wakifika bongo mnaanza kuwapanga wapunguze mishahara! Nna ushahidi wa kutosha wa ma HR wenye roho za chawa kama Hawa.Sio POA umasikini wangu ndio umasikini wako.
Muanzisha Uzi una nafasi Yako peponi.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app