Uzi maalum kwa wale tunaoshindwa kufanikiwa kimaisha hata tukipata hela zinayeyuka

Uzi maalum kwa wale tunaoshindwa kufanikiwa kimaisha hata tukipata hela zinayeyuka

buzitata

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2017
Posts
2,370
Reaction score
7,900
habarn wakuu

Katika maisha suala la kufanikiwa (kuwa na maendeleo) huwa lina mambo mengi sana, kuna wakati unaweza kupata pesa nyingi Ila linapokuja suala la kuwekeza ili pesa ijizalishe au kuwa na vitu fulani huwa kuna changamoto zake jambo linalopelekea kuendelea kuishi maisha yale yale

Nije kwa upande wangu Mimi
Nilivomaliza chuo ngazi ya Diploma nikasema ngoja nipige kadegree, nikiwa mwaka wa pili nilibahatika kupata kazi ya melini (oiler) kwenye nchi fulani kwa hiyo nikaamua kuacha chuo

Nikavuna pesa nzuri tu ya kuweza kununua vitu fulani Ila sijui niliingiwa na pepo gani nikasema hii hela ngoja niitupe kwenye elimu nikasome short course Kama tano hivi ili nipate sifa ya kufanya mtihani wa office in charge of engineering watch (wale wa melini watakua wamenielewa hapa)

Basi ile kurudi tu kweli nikaanza michakato ya kusoma ila kuna upepo fulani hivi ulinipitia wa uvivu kila siku nikawa najisemea nitaanza wiki ijayo wakati huo pesa inazidi kupungua tu kuja kushtuka hivi nimebakiwa na pesa ambayo haiwezi kukidhi masomo niliyotaka kusoma nikajisea aaah ngoja niachane nayo nitafanya safari ijayo, kumbuka hapo sijanunua kitu chochote zaidi ya nguo tu na kula bata kila sehemu za starehe zilipo, ikafika hatua pesa zote zimeisha na kurudi kazini ilikuwa tabu sana kwa sababu kampuni ilipunguza wafanyakaz hivyo kupelekea nafasi yangu ya kurudi isogezwe mbele kama miezi mitatu hivi, Maisha yalikuwa magumu sana zaidi ya sana,

Mungu akanibariki nikaondoka tena

Nikavuna pesa kama kawaida ila safari hii nikasema afe kipa afe beki Ila lazima nisome

Kweli nilivyorudi sikuchelewa na 75% ya pesa nikaitupa kwenye elimu nilikuwa bize hatari nikajisahau tena kununua hata kakiwanja ila nilikuwa ninajipa moyo tu kwamba sasa hivi nina tiketi mkononi siku ikifika mimi ni kukwea pipa tu

Nilivomaliza mitihani yangu namshukuru Mungu nilitoboa sasa nikawa kama nimejisahau fulani hivi kale katabia ka starehe kakarudi tena nikaanza kutumbua kale kapesa kalikobaki,. Siku ya kuondoka ilivokaribia crew coordinator wangu akanambia wanacancel tiketi kwa sababu ya Corona😠😠😠😠 imagine pesa niliyorudi nayo yote hakuna Cha maana nikichofanyia zaidi ya kusoma tu

Sasa hivi nipo tu nitaangalia mtandaoni kuhusu habari za Corona na update za kufunguliwa airport ya huko ninakokwenda

Tupe na wewe kitu kinachokufanya usifanikiwe hata pindi unapopata pesa za kuweza kuleta maendeleo
 
Ulikuwa unafuna vitumbua tu.....
wala hujapoteza hela ume-enjoy....
katafute nyingine
 
Mm Kuna katabia Niko nakafanyia research ndogo nijue kanatokana na nn na Ni jins gani naweza kukaepuka.


KUVUNJA KIBUBU KABLA YA MUDA WA MALENGO

KUTUMIA HELA YA AKIBA TOFAUTI NA MALENGO NILIYOJIWEKEA
 
Simply mleta uzi ulikosa discipline katika matumizi ya hela yako, ila habari njema ni kwamba pesa ile ulitumia kuenjoy ama kwa lugha nyingine kula bata, yes! Hapo hakuna kilichoharibika, kimfaacho mtu chake. 😅
 
Simply mleta uzi ulikosa discipline katika matumizi ya hela yako, ila habari njema ni kwamba pesa ile ulitumia kuenjoy ama kwa lugha nyingine kula bata, yes! Hapo hakuna kilichoharibika, kimfaacho mtu chake. 😅
Mkuu omba mungu yasikukute tu
 
mimi nilikuwa kwenye ushetani huo miaka 4 nilivyoajiliwa salary ilikuwa napiga mitungi after few days ela inakwisha maendeleo amna nilipshtuka mpaka Mungu aingilie kati lakini ni lazima upitie hivyo ili ukija kukaa sawa uzingui tena,nilinunua kiwanja ni kakaa miaka 3 bila hata kuweka tofali kwa sababu ya bata any way tushtuke muda unakwenda sana
 
Kujifunza kuwekea kila hela malengo ni jambo la msingi
Ukiona umeahirisha lengo na huna biashara ya kuwekeza basi iwahishe kwenye akiba maalumu isikushawishi
Akiba haiozi!
 
Kujifunza kuwekea kila hela malengo ni jambo la msingi
Ukiona umeahirisha lengo na huna biashara ya kuwekeza basi iwahishe kwenye akiba maalumu isikushawishi
Akiba haiozi!
fixed account ndio mkombozi hata ukiwa na shida ya kufa uitoi
 
Back
Top Bottom