Uzi maalum kwa wale tunaoshindwa kufanikiwa kimaisha hata tukipata hela zinayeyuka

Uzi maalum kwa wale tunaoshindwa kufanikiwa kimaisha hata tukipata hela zinayeyuka

Mwezi wa 12 mwaka Jana 2019 nilipata millioni 3 cash ikaisha tu pasipokujua imeishaje ndani ya mwezi moja ikaja tena mwezi wa NNE mwaka huu nilienda mafunzo flani ya kikazi nilikaa mwezi moja Nikamake 3 millions kutokana na allowances hadi saivi sijui hata zimeishaje wandugu sijajua nafeli wapi...mwezi huu wa 6 nategemea malipo flani kazini ambayo itakuwa Ni 2 millions kama bonus nishapanga niingize kwenye biashara ya dagaa lakini na yenyewe sijui kama itatimia ndoto
 
habarn wakuu

Katika maisha suala la kufanikiwa (kuwa na maendeleo) huwa lina mambo mengi sana, kuna wakati unaweza kupata pesa nyingi Ila linapokuja suala la kuwekeza ili pesa ijizalishe au kuwa na vitu fulani huwa kuna changamoto zake jambo linalopelekea kuendelea kuishi maisha yale yale

Nije kwa upande wangu Mimi
Nilivomaliza chuo ngazi ya Diploma nikasema ngoja nipige kadegree, nikiwa mwaka wa pili nilibahatika kupata kazi ya melini (oiler) kwenye nchi fulani kwa hiyo nikaamua kuacha chuo

Nikavuna pesa nzuri tu ya kuweza kununua vitu fulani Ila sijui niliingiwa na pepo gani nikasema hii hela ngoja niitupe kwenye elimu nikasome short course Kama tano hivi ili nipate sifa ya kufanya mtihani wa office in charge of engineering watch (wale wa melini watakua wamenielewa hapa)

Basi ile kurudi tu kweli nikaanza michakato ya kusoma ila kuna upepo fulani hivi ulinipitia wa uvivu kila siku nikawa najisemea nitaanza wiki ijayo wakati huo pesa inazidi kupungua tu kuja kushtuka hivi nimebakiwa na pesa ambayo haiwezi kukidhi masomo niliyotaka kusoma nikajisea aaah ngoja niachane nayo nitafanya safari ijayo, kumbuka hapo sijanunua kitu chochote zaidi ya nguo tu na kula bata kila sehemu za starehe zilipo, ikafika hatua pesa zote zimeisha na kurudi kazini ilikuwa tabu sana kwa sababu kampuni ilipunguza wafanyakaz hivyo kupelekea nafasi yangu ya kurudi isogezwe mbele kama miezi mitatu hivi, Maisha yalikuwa magumu sana zaidi ya sana,

Mungu akanibariki nikaondoka tena

Nikavuna pesa kama kawaida ila safari hii nikasema afe kipa afe beki Ila lazima nisome

Kweli nilivyorudi sikuchelewa na 75% ya pesa nikaitupa kwenye elimu nilikuwa bize hatari nikajisahau tena kununua hata kakiwanja ila nilikuwa ninajipa moyo tu kwamba sasa hivi nina tiketi mkononi siku ikifika mimi ni kukwea pipa tu

Nilivomaliza mitihani yangu namshukuru Mungu nilitoboa sasa nikawa kama nimejisahau fulani hivi kale katabia ka starehe kakarudi tena nikaanza kutumbua kale kapesa kalikobaki,. Siku ya kuondoka ilivokaribia crew coordinator wangu akanambia wanacancel tiketi kwa sababu ya Corona😠😠😠😠 imagine pesa niliyorudi nayo yote hakuna Cha maana nikichofanyia zaidi ya kusoma tu

Sasa hivi nipo tu nitaangalia mtandaoni kuhusu habari za Corona na update za kufunguliwa airport ya huko ninakokwenda

Tupe na wewe kitu kinachokufanya usifanikiwe hata pindi unapopata pesa za kuweza kuleta maendeleo
Pole sana Chief, saizi umeishajua kosa mambo yakiwa vizuri huwezi kurudia kosa.

Kama umepiga Oral na umechukua CoC tafuta sehemu jishikize unaposubiri corona ipite.

Wenzako imetubidi tupambane na meli za barabarani na kung'oa mihogo tukijipanga kurudi baharini.
 
Hahaha mkuu COC tayar ninayo na nimejitupa mwanza nikiskilizia corona ikate ninyanyue nanga
 
nilipata 50m .....25m nikanunua viwanja viwili tofauti vya nyumba na kuweka misingi ... 5m bata , 20m ikazama kwenye kilimo,forex na mambo mengine ya online yanayofanana nayo..pambaf kabisa....sasa mwaka wa tatu natumbua macho kwenye ile misingi miwili ya nyumba
Dah..forex , kilimo,
 
Mwezi wa 12 mwaka Jana 2019 nilipata millioni 3 cash ikaisha tu pasipokujua imeishaje ndani ya mwezi moja ikaja tena mwezi wa NNE mwaka huu nilienda mafunzo flani ya kikazi nilikaa mwezi moja Nikamake 3 millions kutokana na allowances hadi saivi sijui hata zimeishaje wandugu sijajua nafeli wapi...mwezi huu wa 6 nategemea malipo flani kazini ambayo itakuwa Ni 2 millions kama bonus nishapanga niingize kwenye biashara ya dagaa lakini na yenyewe sijui kama itatimia ndoto
una tatizo spritually , tafuta matibabu mapema kabla hujaendelea kuteseka
 
Back
Top Bottom