Uzi maalum kwa wale wanaomuamini Mungu muumba

Uzi maalum kwa wale wanaomuamini Mungu muumba

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
4,781
Reaction score
14,415
Good day, Good people!

Hivi Karibuni kumezuka mfululizo wa nyuzi kibao hapa JF na zote zikipinga uwepo, uweza, na utendaji kazi wa Mungu. Kiukweli zimenifanya nikazama ndani kufikiri kwa kina zaidi juu ya uwezo wa Mungu na nimepata haya ya kuzungumza na kushare na nyinyi kidogo, ila ningependa kuona na nyie mkiandika sababu zinazowafanya kuamini Mungu yupo na ndie aliezitanda mbingu na nchi.

Iko hivi, Miaka michache iliyopita kumekuwa na wimbi la wanasayansi nguli waliokuwa "notorious atheist"(kindakindaki wasioamini mungu kabisa) kwa miaka kibao kuanza tena kuamini, kukubali na kukiri uwepo wa Mungu hadharani ila tukio maarufu zaidi lilikuwa la mwanasayansi mashuhuri alieshawishi watu wengi zaidi wamkane Mungu kuamua kumgeukia Mungu na kuandika kitabu nilichoambatanisha hapo chini jamaa anaitwa Mr Antony flew kuamua kukiri kwamba namnukuu "God exist and he is the master of the people and universe" But sababu kubwa kwao ilikuwa ni wao kutoka nje ya Dunia na kujionea maajabu mengi lukuki ambayo yaliwalazimu kuamini namna universe and Earth zinavyofunction kwa namna ya kustaajabisha yenye kufuata utaratibu naalumu wa laws and regulation za ajabu basi wakakiri kuna mystic higher spirit ambae ni best designer ever wao wanamwita "supreme being" mwenye uwezo wa ajabu sana, maana walichokiona ni kila kitu kinafanya kazi kwa mfumo wa laws of nature ambazo zina viashiria vya kuwekwa na mtu/roho kubwa maana haviwezekani kujipangilia vyenyewe katika usahihi wa kimfumo kama vile na kufuata utaratibu kwa usahihi kwa mabilion ya miaka bila kuparaganyika au kujikanganya. Cha kwanza;

Earth distance
Hawa wanasayansi waligundua kuna umbali sahihi kabisa Kati ya jua na Dunia.. Na ingetokea Dunia ingesogea kidogo kuelekea jua lilipo basi Dunia ingeungua sana na pia ingetokea Dunia ingesogea mbele kidogo tu kuliacha jua basi Dunia ingekuwa na barafu jingi sana Kwa kukosa joto na isingeruhusu maisha yawepo lakini kaiweka umbali sahihi na lilipo jua ili ipozwe na kuchemshwa na jua la wastani. Haiwezi kutokea out of nowhere there must be designer wa kufanya hizi complex and sophisticated calculation. Na pia unajua dunia ikisimama kwa sekunde moja inakuwaje? Wote tutavurumushwa hadi kwenye sayari ya Jupiter tukafie huko maana inatembea kwa kasi...but kwa miaka dahari Dunia haijawahi kusimama maana ikisimama Kwa kasi inayoenda basi miili yetu itaokotwa Jupiter. Sijui unanielewa hapa!? Ni kwa huruma tu ya Mungu anaiacha inazunguka dearly kwa Upendo wake for billions of years. Ninashukuru Mungu kwa hili.

Earth size
Sikia hii unajua kwamba hii size ya dunia ndio sahihi na salama kwa maisha yetu sababu inafanya dunia iwe na mchanganyiko sahihi wa gas za oxygen na nitrogen kiasi kinachosuport maisha Duniani hili viumbe tuishi. Dunia ingekuwa ndogo tu basi kungekuwa na kiasi kikubwa sana cha hydrogen hivyo kusababisha maisha yasiwezekane hapa Duniani. Kama ambavyo ukienda mile 50 juu ya uso a dunia huipati hii perfect gas mixture ya Duniani. Hayajajileta haya yote kafanya Mungu wetu kwa uweza wake mkuu sana.

Brain,
Ubongo unavyofanya kazi unathibitsha jinsi Mungu alivyo na uweza wa ajabu...unajua ubongo unachakata taarifa zaidi ya million kwa sekunde kwa wakati mmoja yaani simultaneously. Haya ni maajabu yaliyopitiliza akili na uwezo wa kibinadamu kufahamu nini kisababishi cha haya yote. Maana ubongo unaweza kuwa unafiri kingine, then hapo hapo ubongo unapima mapigo ya moyo, unapima temperature ya pale chini ulipokanyaga, unatafsiri harufu mbalimbali, e.t.c

DNA code informs,
Hii ndio imewafanya kila mtaalamu Duniani anaesoma biology kushangaa akili kubwa isiyomithilika iliyotumika kwenye Ku code zile DNA kwenye cell maana kila cell ina billion of DNA zilizokuwa coded kwa usahihi na uwezo wa hali ya juu zikitunza taarifa za kila mmoja kwa usahihi Zinazothibitsha kuna kazi ya akili sana imefanyika...nani nafanya hapo sasa ndio wanasayansi wanarudi mezani na kukiri uwepo wa "mystical supreme spiritual being" God, Wanakwambia hata tupewe miaka billion hatuwezi kufanya coding ya DNA hata kwa mtu mmoja kamwe na hakuna kiumbe binadamu aliezaliwa na mwanamke anaeweza kufanya hii kazi. Nani kafanya sasa hii kazi..wenyewe huwa wanajijibu kwamba "there is supreme being spirit" who coded this DNA. Maana hata kwenye computer lazma kuwe na mtu wa kufanya code ili computer ifanye kazi unless hautakuwa computer...!

Na maelezo ya DNA yanathibitisha Mungu anatujua sote zaidi tujijuavyo sisi wenyewe maana kila mtu kamuumba kwa utofauti wa kipekee sana. Tumuheshimu Mungu.. Kuna jamaa humu alimwita eti "Mungu zuzu" C'mooooon guys hiki kiburi cha maisha ya Duniani kisitupe jeuri ya kumdhiaki na kumtukana Mungu...tumuheshimu Mungu!! kama baba yako tu asie na uungu wowote anataka heshima basi hopefully Mungu atakuwa zaidi yake...let give him thanks and praises he won't deceive us.

Hayo ni baadhi tu, kuna mengi yanayo tuthibitishia Mungu anaishi...ana uweza..na yupo.

View attachment 795233View attachment 795234View attachment 795235View attachment 795236
 
Mungu muweza wa yote, mwenye mapenzi kemkem, aliyepo mahali kote kwa wakati wote, na tararira zingine kama hizo, mpaka hivi sasa mungu huyo hakuna ushahidi wa uwepo wake.

Hilo mkubali mkatae, ndo ukweli wenyewe huo.

Huyo mungu mnayedai yupo anafeli mitihani midogo na myepesi sana ya maswali ya kawaida kabisa.

Jana/ leo imeletwa habari humu kuwa kuna mchungaji huko Ethiopia kauliwa na mamba ziwani alikokuwa anawabatiza sijui waumini wake wale.

Huyo mchungaji alikuwepo hapo ziwani akifanya kazi ya ki-mungu. Na nadhani ni haki nikimuita huyo mchungaji kuwa ni 'wakala' wa mungu.

Sasa huyo mungu alikuwa wapi kumnusuru kifo huyo 'wakala' wake? Iweje huyo mungu akampa akili na uwezo huyo mamba wa kumshambulia huyo 'wakala' wake huko ziwani hadi kumuua?

Sijawahi hata kuparuriwa na paka lakini nadhani kung'atwa na mamba hadi ufe kunauma kweli kweli.

Huyo mungu alishindwa nini kumnusuru huyo 'wakala' wake kuepuka hayo maumivu?

Ukweli ni kwamba mpaka hivi sasa hakuna ushahidi wa huyo mungu. Kilichopo ni mambo ya kufikirika tu, au waweza kuyaita 'imani'.

Kwa hiyo, kwangu mimi, mpaka hivi sasa huyo mungu ni kiumbe msasili [mythical figure].

Hakuna ushahidi unaothibitisha, unaotosha, na unaohitimisha kuhusu uwepo wake.
 
Ngoja kwanza nivute hii pumzi ya Bure kabisa nione watu wanavyojikanyaga hapa.

Kibaya zaidi mtu akiugua tu kajipu akaanza kushindwa kufanya ujeuri wake kwenye mgongo wa Ardhi, utamsikia anasema ''Mungu nisaidie" Mungu yupi unayemuomba akusaidie ilihali huamini uwepo wa Mungu?.
 
Ngoja kwanza nivute hii pumzi ya Bure kabisa nione watu wanavyojikanyaga hapa.

Kibaya zaidi mtu akiugua tu kajipu akaanza kushindwa kufanya ujeuri wake kwenye mgongo wa Ardhi, utamsikia anasema ''Mungu nisaidie" Mungu yupi unayemuomba akusaidie ilihali huamini uwepo wa Mungu?.
Ajabu gani hii,."Mungu nisaidie" wakati huohuo wanajifanya hawaamini...mbona hawasemi mbuzi/punda/mti niokoe...?;
 
Mungu Yupo.
Muumbaji wa mbingu na nchi na vyote vizijazavyo wakiwepo na hao atheists.
Kuamini hayupo hakuondoi uwepo wake. Ni sawa na mtu kufumba macho mchana alafu atake kushawishi watu wanaoona mchana ni usiku kumbe yeye ndiye haoni na anajua kwa nini haoni.
 
Back
Top Bottom