Mungu muweza wa yote, mwenye mapenzi kemkem, aliyepo mahali kote kwa wakati wote, na tararira zingine kama hizo, mpaka hivi sasa mungu huyo hakuna ushahidi wa uwepo wake.
Hilo mkubali mkatae, ndo ukweli wenyewe huo.
Huyo mungu mnayedai yupo anafeli mitihani midogo na myepesi sana ya maswali ya kawaida kabisa.
Jana/ leo imeletwa habari humu kuwa kuna mchungaji huko Ethiopia kauliwa na mamba ziwani alikokuwa anawabatiza sijui waumini wake wale.
Huyo mchungaji alikuwepo hapo ziwani akifanya kazi ya ki-mungu. Na nadhani ni haki nikimuita huyo mchungaji kuwa ni 'wakala' wa mungu.
Sasa huyo mungu alikuwa wapi kumnusuru kifo huyo 'wakala' wake? Iweje huyo mungu akampa akili na uwezo huyo mamba wa kumshambulia huyo 'wakala' wake huko ziwani hadi kumuua?
Sijawahi hata kuparuriwa na paka lakini nadhani kung'atwa na mamba hadi ufe kunauma kweli kweli.
Huyo mungu alishindwa nini kumnusuru huyo 'wakala' wake kuepuka hayo maumivu?
Ukweli ni kwamba mpaka hivi sasa hakuna ushahidi wa huyo mungu. Kilichopo ni mambo ya kufikirika tu, au waweza kuyaita 'imani'.
Kwa hiyo, kwangu mimi, mpaka hivi sasa huyo mungu ni kiumbe msasili [mythical figure].
Hakuna ushahidi unaothibitisha, unaotosha, na unaohitimisha kuhusu uwepo wake.