Uzi maalum kwa watu wanaohitaji kuagiza magari, ama wenye malengo ya kuagiza magari

Karibuni kwa maswali.
Je huwa wanauplift kodi au inayoonekana kwenye calculator ya tra ndio hiyo hiyo? Swali hili sio la nadharia bali la uzoefu ikiwa tu unazoefu. Mfano unaweza angalia gari online cif yake $10,000 lakini ukiingiza kwenye kikotoo inaonyesha kodi ambayo ukiangalia cif kwenye kikokotoo ni $6,000, kwakuwa kikotoo hakiangalii bei bali aina ya gari, mwaka n.k, Huko nyuma walikuwa wanauplift ushuru kuendana na cif halisi, je sasa hivi ikoje.
 
Hello, kuhusu swali kama lako, nililitolea ufafanuzi hapo juu.
 
Salama mkuu,
Corolla Runx ya mwaka 2004 na 2006 (1.4L) ambayo mileage yake ni kati ya Km 90k to 120k.
 
Wooohyy
 
Mheshimiwa rais aliangalie hili angalau gari ya 5m ushuru uwe 2.5m.
 
Mi nahitaji kununua Nissan Civilian, nimechunguza nikaona zinaanzia Mil 40...tatizo ni kwamba mm nina Mil 20 tu. Naombeni ushauri nifanye je ..maana ninaihitaji haraka aisee.
 
Hello,

ahsante kwa swali.

Gharama za kuiagiza hadi kufika bandari ya Dar es salaam ni $2,874 ambayo ni sawa na TZS 6,897,600/=

Ushuru TZS 5,679,000/=

( Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System )

Gharama za matumizi ya bandari, D O, Shippingline pamoja na agent utakae mtumia kukutolea gari lako hazitozidi TZS 800,000/=

Hivyo, jumla itakua kiasi cha

TZS 13,376,600/= (Hapo hadi wanakukabidhi mikononi mwako)

comprehensive insuarance yake watakutoza TSHS 553,000/=

JUMLA KUU : TZS 13,929,600/=

Ahsante.
 
Mi nahitaji kununua Nissan Civilian, nimechunguza nikaona zinaanzia Mil 40...tatizo ni kwamba mm nina Mil 20 tu. Naombeni ushauri nifanye je ..maana ninaihitaji haraka aisee.
Nina shida Kama yako.. Ila Mimi nikwenye kujenga! Nina milioni 35 Ila QS amesema nahitaji milioni 70 kumaliza nyumba. Nahitaji kuamia haraka! Ukimpata mtu wakukusaidia niunganishe na mimi.
 
Nina shida Kama yako.. Ila Mimi nikwenye kujenga! Nina milioni 35 Ila QS amesema nahitaji milioni 70 kumaliza nyumba. Nahitaji kuamia haraka! Ukimpata mtu wakukusaidia niunganishe na mimi.
Hello, sina uhakika sana kama suala hili umeliwasilisha kwenye uzi sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…