Uzi maalum kwa watu wanaohitaji kuagiza magari, ama wenye malengo ya kuagiza magari

Karibu kwa maswali!!

Habari, naomba utoe elimu kwa mtu ambae hajawah kuagiza gari lakini anataka kuagiza gari kwa mara ya kwanza.

Sio kutumia waagizaji magari, yaani kuagiza mimi kama mimi. Mambo ya kuzingatia ili gari ifike kwa usalama n.k
 
Mkuu Suzuki jimny ya mwaka 2005>> 1.3L ina gharama kiasi gani.
Compared with
Suzuki jimny ya 660cc ! 2005
 
Habari, naomba utoe elimu kwa mtu ambae hajawah kuagiza gari lakini anataka kuagiza gari kwa mara ya kwanza.

Sio kutumia waagizaji magari, yaani kuagiza mimi kama mimi. Mambo ya kuzingatia ili gari ifike kwa usalama n.k

Sawa sawa, nitakuwekea hapa
 
Kuna jamaa yangu anatamfuta mtu amuuzie ist,ameiagiza from japan imefika bandarini pesa ya kugombolea ni kama 6m,yeye ameiagiza kwa kama 5m!
Anatafuta mtu amrudishie hiyo 5m then yeye achukue hiyo ist mpya
Namba zake ni 0736770052
acha utapeli mkuu
 
Sasa kama imeuzwa tayari ni sawa, mambo ya kulengeshana
 
Umekosea sana kuniita tapeli
Hunijui sikujui ungeniuliza tu kistaarab alafu ungeona sielewek ndo uje hapa useme mimi tapeli
Umenikosea sana sana
Sasa mkuu nikuombe msamaha kwa lugha nyepesi, samahani! ww na mimi tunaeza kuwa tunatafuta riziki lakini hivi sasa watu waaminifu wamepungua sana, umakini ni lazima na uangalizi wa mali wa hali ya juu. siku hizi hawa matapeli wamekuwa wakifariji wateja kwa lugha nzuri kumbe siyo.
 
Naomba kuulizia inagalama gn gali hii mpaka kuipata mkononi,Mitsubishi lancervan ya mwaka 2014. Ina cc 1490
 
Nahitaji gari ya kishua yenye space nzuri na ulaji wa mafuta mzuri ambayo naweza enda nayo shamba au starehe bajeti 12m kwa kila k2
 

Habari ruli


Manunuzi (Hadi bandari ya Dar es salaam

$2,383 = TZS 5,719,200/=

Ushuru = Nashindwa kukupigia hesabu maana kwenye system yao haijaorodheshwa. hivyo hadi kufanya mawasiliano nao. (Kwa makadirio inaweza kufika 8.5mil) Hayo ni makadirio na sina uhakika kwenye hilo. Hivyo ni vyema uwasiliana nao.

Mengineyo (utoaji wa gari, shippingline , DO , agent atakae toa gari) hatozidi 850,000/= kwa vyote.
 
Hello,

Haina neno iliniweze kukupa hesabu halisi. Ni vyema ukanionyesha gari unayoihitaji (gari halisi) kisha ndio nikakupa mchanganuo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…