Pre GE2025 Uzi maalum wa hali ya kimtandao kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025. Intaneti itapatikana au itazimwa kama 2020?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Wakuu

Wote tunakumbuka kipindi cha Magufuli mambo yalivyokuwa.

Baada ya purukushani zake za kutishia wapinzani, kuzorotesha uchumi na mwisho kuona majority ya watanzania hawamkubali zikaanza figisu za kutuminya kipindi cha Uchaguzi.

Sijui alikuwa na wasiwasi wa nini?

Uchaguzi mkuu ulivyofika akazima internet baada ya kuona kila mahala kapata kura kiduchu na kura feki za kumnusuru zinazosambazwa na vijana wake zinarekodiwa kwa simu na kurushwa mitandaoni.

Sasa ni zamu yake Rais Samia.

Muda umefika wa yeye kujua rangi halisi za watanzania. Hivi kweli tutatoboa kipindi cha Uchaguzi bila kuzimiwa Intaneti?

Ukizingatia mambo kama tozo, DP World, mgawo wa umeme, kuhamishwa kwa Wamasai wa Ngorongoro, kufukuzwa kwa Wamasai wa Loliondo, rushwa na upigaji serikalini, kukopa mikopo kuliko kithiri.

Hivi kweli rais Samia hatazima internet kwenye uchaguzi ujao?

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

SOMA PIA

 
Atajuta huyu Bi U....s...hungi
 
Mpaka azime internet anamuogopa nani wakati Wapinzani wake wote mpaka sasa wapo hoi?
Labda tusubiri 2025 lakini kwa sasa Wapinzani wote wapo ndembendembe wamechoka
 
Msiojua kwa ujinga wenu msipopiga KURA mnawapa ahueni ccm kuliko mkipiga kwasababu nature haikubali vacuum kwahiyo ombwe litajazwa tu na kubalansi nature.
Kupiga kura ambayo haina impact yoyote kwenye matokeo, ni matumizi mabaya ya raslimali muda. Mtu mwenye muda wa kupoteza tu ndio ataenda kushiriki huo upuuzi.
 
Akiwa wa habari ni wahabari miezi 3 kabla na tatu baada zalima viumanešŸ˜Ž
 
Kupiga kura ambayo haina impact yoyote kwenye matokeo, ni matumizi mabaya ya raslimali muda. Mtu mwenye muda wa kupoteza tu ndio ataenda kushiriki huo upuuzi.
Ile miswada 3 inayopelekwa bungeni bado unaona haitakuwa na msaada wowote kwenye kutenda haki ktk chaguzi?
 
Ile miswada 3 inayopelekwa bungeni bado unaona haitakuwa na msaada wowote kwenye kutenda haki ktk chaguzi?
Hakuna chochote kitafanyika, ule ni usanii kama usanii mwingine. Hiyo miswaada mitatu yenyewe imekwepa matakwa halisi ya vyama vyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…