Uzi maalum wa kupeana faraja hasa tuishio mbali na familia zetu. Tukitafuta Maisha ya kesho

Uzi maalum wa kupeana faraja hasa tuishio mbali na familia zetu. Tukitafuta Maisha ya kesho

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Habari wanajf. Binafsi Niko visiwa vya Haiti Marekani ya kaskazini. Kiujumla Maisha ndio yalinifanya nikafika huku, kwa sikuwahi kuwaza kuwa ntavuka visiwa vyetu vya Tanzania Yaani Pemba na Unguja.

WATU WA HUKU(WAHAITI)
Watu wa huku ni weusi ti Kama sisi huwezi kutofautisha na wasukuma, wanyakyusa na makabila mengine ya kibantu, Huku mapinduzi ya serikali nje nje, majanga ya asili Kama tetemeko na kimbunga vilishazoeleka.

Hakika ndio maana wamejaa weusi tu. Maisha Ni Kama ya uswahilini tu. Nakusihi na kukutia moyo uliyeko mbali na familia yako ukiipambania ili Mungu akijaali waishi vyema usikate tamaa licha ya changamoto unazipitia na upweke wa kuwa mbali na familia Mungu yu pamoja nawe.

Tulizimis familia zetu tukiwa mbali nazo tuziombe na kushirikiana nazo katika riziki tujaliwazo tusizitelekeze. Naomba kuwasilisha. Wasalimu Tanzania.

Karibuni Haiti.
 
Sasa si utume picha na video, ulimwengu wa Sasa Raha ya ushahidi uwe na picha au video 😁😁😁😁😁😁
 
[emoji478][emoji478]
JamiiForums68569125.jpg
 
Pole na hongera kwa kupambana kifupi mimi siwezi kuwa mbali na familia kiasi hicho uko si ndo kunamachafuko uko??
 
Unatoka lwa poorest country ina the world unaenda kwa one of the poorest countries in the world,. Anyway, maisha yanasakwa popote.
 
Vipi na sisi ambao wapendwa wetu wapo mbali? Naona tunashahabiana katika hilo.
Ni hali ngumu sana kupitia, pole Mkuu.
 
Back
Top Bottom