Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
TAHADHARI KWA WALE WENYE MAGARI DAR ES SALAAM. Kuna mzee mmoja wa makamo hivi, hupenda kuvaa kanzu, midomo yake imeungua kidogo. Mzee huyu ni MWIZI na JAMBAZI. Jinsi anavyofanikisha uhalifu wake: Huwa anavizia waendesha magari (mara nyingi kinamama) hasa yanapokuwa kwenye mwendo mdogo. Yeye hujibamiza upande wa kushoto na kisha hujidondosha chini kwa kisingizio kuwa amegongwa. Kutokana na kitendo hicho kuwa cha ghafla sana, wanaoshuhudia na mwenye gari pia huamini ni ajali kweli! Anaponyanyuka hufunua kanzu yake na kuonesha mirija ya mpira na mfuko wa sandalusi aliyofungwa kama mgonjwa wa kibofu cha mkojo na kudai yeye ni mgonjwa na anaelekea hospitali na umemgonga. Hukutajia hospitali iliyo karibu na mahali "ajali ilipotokea" na kuelekeza apelekwe huko, na akiingia kwenye gari - na huandama na kijana - ama hudai fedha akajitibu mwenyewe au hutoa bastola na kuwapeleka madereva Wazo Machimboni - nyuma ya kiwanda cha saruji, Ununio kulikokuwa machimbo ya mawe zamani ambako sasa hivi kumebaki mashimo tu au Mla Mlaleni nyuma ya Kongowe, na kuwapora wahanga wake kila kitu - pamoja na funguo za gari!. Ikitokea mwenye gari hukusimama baada ya "ajali" mzee huyo hukodisha pikipiki na kuifuata gari yako hadi utakapo-park. Maeneo ya mawindo ya mzee huyo ni: jirani na Central Polisi/Railway Station, Posta Mpya, Jangwani kutokea club ya Yanga kuelekea Kigogo Darajani, Hospitali za Mwananyamala, Temeke, Mnazi Mmoja, Ubungo Stand na Gongo la Mboto. Mara nyingine pia hupenda kukaa njia panda/kona ya Barabara ya Migombani na ile ya Mwai Kibaki (old Bagamoyo road - Zantel). Tuchukue tahadhari, na inapowezekana toa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi. NAKUOMBA UISAMBAZE TAARIFA HII KWA WENGINE!!!! MSIJE KUSEMA SIKUWAONYA!!!!?????
 
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…