Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mume alichomjibu mchepuko wa mke wake

_ Jamaa kamuaga mkewe anaenda semina Songea kwa wiki nzima kumbe kahamia kwa demu nyumba ya pili toka kwake. Siku ya 1 kalala asubuhi alipoamka kachungulia kwake kukoje,

si kamuona jamaa yuko nje ya nyumba yake kavaa taulo lake anapiga mswaki. Akapiga kelele, 'We nani?', Jamaa akajibu, 'Mshikaji mambo ya mjini, mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea mi ndo najivinjari hapa'. Mume kajibu kwa uchungu, Shenzi mkubwa, ngoja nirudi toka Songea nakuua.
Hahaaa dooh
 
Mtoto: Baba mie naenda kulala

BABA: Kunywa kabisa maji hyo tabia yako ya kuita mtu akuletee maji ya kunywa chumbani sitaki kuisikia

MTOTO : Baba mie sina kiu leo

BABA: We haya ila Leo ntakukomesha tabia yako!

******Baada ya dakika kadhaa*****
MTOTO; Anaita Babaaa babaaa we babaaa

BABA: nn wewe na makelele yako?

MTOTO: Niletee maji ya kunywa

BABA: Nilikuambiaje? Si ulijifanya husikii kiu sasa nikija huko nakuja kukuchapa

MTOTO: Ukija kunichapa uje na maji ya kunywa!
 
Mke wako anarudi nyumbani kasuka nywele za 30,000 na hujampa hata mia,we unakalia kusema waooo waoooo kama king'ora cha ambulance.
Shauri yako we endelea kusema waoooo waooo na atakuwa wao kweli
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji9] [emoji9] [emoji9] [emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji7] [emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6] [emoji6]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake banaaaa... Tusaidie Baaba

Jamaa kaamka asubuhi kavaa track suit akamuamsha mkewe
MUME:Amka twende jogging mke wangu?

MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa?

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya.

MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?

MUME: Basi yaishe endelea kulala

MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?
MUME:Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby
MKE:Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?
MUME:Jamani mi sijasema hilo
MKE:Kwa hiyo mie muongo?
MUME:Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii
MKE:Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?
MUME:Sikia we lala mie naenda jogging.
MKE:Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"
MUME:Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe......
 
*Nawapenda sana wanawakewa uswahili kwa ubunifu wao.Hivi n baadhi ya vicheko walivyocheka kwenye miaka tofauti.*
2002 to 2004-walikuwa wanacheka "hehehe haloooo"
2005 to 2007-wakaja na "heheheee utajijuuu"
2008 to 2010-wakaleta hii ya "heheheee unalooo"
2010 to 2012-wakaleta "hehehe utajibebaaa"
2012 to 2014-wakaja na "heheheee kaoge"
2014 to 2015-safari hii hapa wakacheka "hehehe chezea mie wewe"
2016 -Hpa ss ndo wamekuja na "...heheheee KANTANGAZEEE.."
2017-Wamekuja na hii hapa hehehee wareree,wapi nyonyo
Je unahisi 2018 watabuni style gani ya kucheka

_Acha niende ivi narudi..._
 
Mtoto kaingia chumbani kwa mama yake ghafla vaaap.
Mama: we Mtoto pumbav sana.... kwa nini unaingia chumbani kwangu bila kupiga hodi??
Mtoto : kwani tatizo nini mama???
Mama : je ukinikuta niko UCHI?
Mtoto: siwez kukukuta uko uchi.
Mama : kwa nini isiwezekane na wakati unajua hapa ni chumbani???
Mtoto: kabla sijaingia huwa nachungulia kwanza kwenye kitobo Cha ufunguo. Nikikukutaga uko uchi huwa siingii.
 
UJUE UMBALI WA KWENDA KWENU

1. DAR - ARUSHA 646 KM
2. DAR - KAHAMA 961 KM
3. DAR - BABATI via moro 876 KM
4. DAR - BARIADI 1127 KM
5. DAR - BUKOBA via kahama 1433 KM
6. DAR - DODOMA 451 KM
7. DAR - GEITA 1228 KM
8. DAR - IRINGA 492 KM
9. DAR - KIBAHA 35 KM
10. DAR - KIGOMA via itigi 1258 KM
11. DAR - KIGOMA via kahama 1476 KM
12. DAR - LINDI 452 KM
13. DAR - MBEYA 822 KM
14. DAR - MOROGORO 192 KM
15. DAR - MOSHI 566 KM
16. DAR - MPANDA via itigi 1383 KM
17. DAR - MTWARA 556 KM
18. DAR - MUSOMA 1370 KM
19. DAR - MWANZA 1152 KM
20. DAR - NJOMBE 710 KM
21. DAR - SHINYANGA 989 KM
22. DAR - SINGINDA 696 KM
23. DAR - SONGEA via moro 949 KM
24. DAR - SONGEA via lindi 1054 KM
25. DAR - SUMBAWANGA 1150 KM
26. DAR - TABORA 829 KM
27. DAR - TANGA 354 KM



Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAISHA NA MAAJABU YAKE[emoji116][emoji116]

Usishangae [emoji15][emoji86]

[emoji86] Mmiliki wa kampuni ya Tecno anatumia iPhone [emoji16]

[emoji86] Kiwanda cha kutengeneza mishumaa kinatumia umeme [emoji16]

[emoji86] Meneja wa kiwanda cha soda anakunywa bia [emoji16]

[emoji86] Aliyegundua pesa alikufa na madeni [emoji16]

[emoji86] Wachina wanatengeneza dawa za kuongeza hips lakini wao wako bapa [emoji16]

[emoji86] Mpenzi wako Mpya ni mpenzi wa zamani wa mwengine [emoji7]

[emoji86] Aliyegundua simu (Alexander Bell) mke wake na mama yake walikua viziwi? Jiulize aligundua ili kumpigia nani? [emoji15]

[emoji86] Kuna watu wameajiriwa ili kufundisha watu wengine namna ya kujiajiri [emoji16]

[emoji86] Baba Mlevi hapendi Mwanawe anywe Pombe! [emoji15]

# Maisha ni Rahisi tu Usijichanganye!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom