Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na yeye aliye juu aliamua ya kuwa wakati, muda na masaa, vyote viwe miliki ya uamuzi wake. Akanena kuwaambia mariisii na madiisii: 'Wakamateni wanipingao, wadhalilisheni wanishaurio, na wawekeni korokoroni wote wanielekezao. Munayo masaa arubaini na manane na hiyo ni ruhusa nawapeni. Nanyi mujuwe ruhusa ya kutoka juu huwa amri.' Nao mariisii na madiisii wakaitika huku wakitikisa mikia: 'Ndio mtukufu jalali. Tumesikia na tunatekeleza!' Basi wakati jua linakwenda machweoni katika siku yake ya pili madhabahuni, akainua bakuli la sadaka kuwataka waamini waingize wenyewe mapato yao. Na huko kwenye mataifa, majela yakajaa, yakafurika na vifua vya waja vikashika mimba za ghadhabu." Amri 23: 1-10
 
Nimepita kwenye kichaka na kukutana na taswira hii ya kufikirisha. Nyuki na nzi wote wametuwa kwenye shada moja la mauwa. Nikajisemea kuwa hatimaye nyuki huyu ataondoka hapa akatumie madini aliyoyakuta kutengenezea asali, na nzi atatumia makinikia kuunda vimelea vya maradhi. Nikajifunza kuwa kwenye maisha, mafanikio hayapo tu kwenye namna fursa ikujiavyo, bali yamo zaidi kwenye namna uitumiavyo. Wahenga walisema: "ukupigao ndio ukufunzao!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…