Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Siasa. Mchezo wa hatari pengine kuliko yote hapa duniani! Aliingia na mikwara kibao akitishia kumfukuza ye yote ambaye angebainika kuwa anavujisha siri za ikulu. Akawatukana Chief Strategist Bannon na Chief of Staff matusi mazito ya nguoni. Leo naye amejikuta kafutwa kazi.Majina mengine si ya kuwapa watoto na ni ya kucheza nayo mbali kabisa. Hili jina la huyu jamaa na makidai yake limemfanya vyombo vya habari vya US vimtangaze in a very negative way, na wala wachekeshaji wa usiku ndiyo wakammaliza kabisa kwa kumuita moochie moochie lol! Pia jamaa kumbe alichukua tizi la kila anapoongea kuongea kama aliyekuwa boss wake.
Mbaya zaidi jamaa alimtelekeza mkewe aliyekuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume tangu ijumaa iliyopita. Hakuwa na mkewe wakati anajifungua na pia hadi hii leo hajamuona mwanae. Mkewe baada ya kuchoshwa na mpuuzi huyu Jumatatu iliyopita alifile for divorce.
Mh! Ndani ya wiki tu unapoteza mke na wadhifa mkubwa na jamii ya Italian Americans wanakung'ong'a na kuomba usingekuwa ni mmoja wao.
Uzuri tu hawa wenzetu karibu wote hawa ni mabilionea na hawana njaa kama hawa wanasiasa wetu uchwara. Zitto hakukosea aliposema kwamba kamwe usimwamini mwanasiasa hata kama ni babako mzazi!