Tambi ni chakula kinachopendwa na wengi...leo tunaanza kwa kujifunza jinsi ya kutengeneza tambi za aina mbalimbali ili kuleta mvuto kwa walaji wa chakula chako. 1.Tambi za soseji Mahitaji: -Soseji -Tambi -mafuta ya kupikia -sukari -maji Jinsi ya kuandaa: *katakata soseji katika vipande vidogo kiasi,soseji moja ikate katika vipande vinne *katika kila kipande cha soseji,chomeka tambi chache *weka katika sufuria na chemsha kwenye maji yenye sukari na mafuta *zikishaiva,pakua na andaa mezani *unaweza kushushia na juisi yoyote ya chaguo lako