Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chakula Kisichodhuru Afya
JE, NI hatari kula chakula? Huenda takwimu zifuatazo zinaweza kufanya mtu afikiri hivyo. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kila mwaka watu milioni 130 hivi katika Eneo la WHO huko Ulaya wanaambukizwa magonjwa
 
Screenshot_2017-08-04-14-00-39.jpg
 
yanayosababishwa na chakula. Katika mwaka wa 1998, zaidi ya watu 100,000 nchini Uingereza walikuwa wagonjwa kwa sababu ya kula chakula kibaya, na 200 kati yao walikufa. Inakadiriwa kwamba kila mwaka watu milioni 76 hivi wanapata magonjwa yanayosababishwa na chakula huko Marekani, na 325,000 kati yao hulazwa hospitalini, na 5,000 hufa.
 
Si rahisi kujua hesabu kamili ya ulimwenguni pote. Hata hivyo, shirika la WHO linaripoti kwamba watu milioni 2.2 hivi walikufa kutokana na magonjwa ya kuharisha katika mwaka wa 1998, na milioni 1.8 kati yao walikuwa watoto. Ripoti hiyo inasema: “Wengi kati ya wagonjwa hao waliambukizwa magonjwa yanayosababishwa na chakula au maji machafu.”
 
Huenda ukashtuka kusikia takwimu hizo kubwa. Lakini je, takwimu hizo zikufanye uwe na wasiwasi mwingi juu ya chakula? Bila shaka la. Ebu fikiria mfano mwingine. Kila mwaka watu milioni 4.2 hivi nchini Australia wanapata magonjwa yanayosababishwa na chakula, yaani watu 11,500 hivi kila siku! Huenda hiyo ikaonekana kuwa idadi kubwa sana. Lakini kwa upande mwingine: Waaustralia hula milo bilioni 20 kila mwaka, kwa hiyo ni milo michache sana inayosababisha magonjwa.
 
Jinsi Vyakula Vinavyosababisha Magonjwa

Jarida la Emerging Infectious Diseases linasema kwamba zaidi ya magonjwa 200 yanaweza kusababishwa na chakula. Hata hivyo, vijidudu vinavyosababisha magonjwa hayo yote si vingi sana. Dakt. Iain Swadling, afisa wa shirika la Huduma ya Kimataifa ya Uchunguzi wa Chakula, anasema kwamba asilimia 90 hivi ya magonjwa yote yanayosababishwa na chakula, huenda yanasababishwa na jamii za vijidudu “zisizozidi 24.” Visababishi vya magonjwa kama vile virusi, bakteria, vimelea, sum
 
Back
Top Bottom