Kile Unachoweza Kufanya
▪ Safisha. Nawa mikono kwa maji ya moto na sabuni kabla ya kuanza kutayarisha kila aina ya chakula. Nawa mikono baada ya kwenda chooni, na baada ya kushughulikia mtoto (iwe ni kumbadilisha nepi au kumpangusa makamasi), au kushika mnyama yeyote, hata mnyama-kipenzi. Osha vyombo, mbao za kukatia, na meza kwa maji ya moto na sabuni baada ya kutengeneza kila aina ya chakula—hasa baada ya kukata nyama, kuku, au samaki na vyakula vingine vinavyotoka baharini. Gazeti la Test linapendekeza “kuosha matunda na mboga katika maji ya uvuguvugu” ili kuondoa wadudu na mabaki ya dawa ya kuua wadudu.