Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pamoja na vyakula vya mafuta, ice cream ni tatizo kwa kuwa ukila sukari unaongezeka uzito bila sababu, pia hujipa msukosuko wakati wa kulala kwa kuwa baada ya muda huyeyuka na kuzaa tatizo nyingine. Aina hii ya vyakula husababisha magonjwa ya kiharusi, kisukari na ugonjwa wa moyo.
 
Kabohaidreti (wanga) kwa wingi au vyakula vyenye sukari kupitiliza

Kundi hili ndilo ambalo watu wengi hulichanganya kwa kuamini kuwa tambi ‘supagheti’ ni chakula chepesi kuliwa usiku, kitu ambacho si sahihi.Tambi ni moja ya vyakula ambavyo havipaswi kuliwa usiku kwani ina wanga mwingi ambao kutokana na kulala hakisagiki na kinaweza kuziba mirija ya damu na kusababisha madhara kwa mtumiaji.
 
Kahawa

Kwa kawaida, kahawa ina kafeini ambayo inaweza kusababisha usumbufu wakati wa kulala kwani hata dawa zenye kafeini hapaswi kupewa mgonjwa mwenye matatizo ya kulala.Vivyo hivyo pia hata soda ambazo zina kafeini, pia zinasababisha mtumiaji kukosa usingizi wa kutosha, hivyo kushindwa kufanya mambo katika mpangilio maalumu siku inayofuata.

Wataalamu wa masuala ya chakula na lishe, Wanasema kuwa kama ni lazima kunywa kahawa, basi iwe ni saa tano au nne kabla ya kwenda kulala.
 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani ya Mfumo wa Chakula Dokta Raymond Mwenesano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili -MNH- anasema kuwa kwa kawaida mwili wa binadamu unapohitaji mapumziko au unapofika muda wa kupumzika inabidi uwe huru kwa maana ya kuwa katika hali ya kawaida, hususan sehemu za ndani kama tumbo.
 
Back
Top Bottom