Kuanzia leo, anza kufikiria kufanya jambo fulani kubwa ambalo hujawahi kulifanya kabla ya hapo, haijalishi watu wengine wataliponda, wataliona dogo au wataona si saizi yako. Unaweza kufanya mambo makubwa ambayo hukuwahi kuyafanya kabla ya hapo. Hiyo ni kwa sababu maumivu yako yamegeuka kuwa nyota ya mafanikio, tumia fikra zako, panua akili yako, jenga na tarajia. Uje na wazo kubwa, jambo fulani kubwa kuliko ilivyo kawaida yako. Tumia fursa yoyote iliopo katika jamii inayokuzunguka, haijalishi upo kijijini au mjini, haijalishi umesoma au la! Labda unahisi kuwa na kipaji fulani, kiboreshe. Songa mbele usikate tamaa mpaka pale matarajio yako yatakapotimia.