Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo, afya ya meno isipopewa kipaumbele, inaweza kusababisha maradhi ya moyo, saratani au hata kuharusi.

Yafuatayo ni mambo 10 ambayo yatakusaidia kufahamu nini utarajie unapokwenda kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno au matibabu ya magonjwa ya kinywa na meno.
 
1- Uchunguzi wa afya ya kinywa na meno hujumuisha uchunguzi wa saratani ya kinywa

Unapokwenda kwa daktari wa kinywa na meno kwa uchunguzi wa kawaida wa kinywa na meno kwa kawaida daktari wa kinywa na meno Inakadiriwa kuwa mtu mmoja hufa kila saa kutokana na ugonjwa wa saratani hii nchini Marekani.
 
2- Magonjwa ya fizi huathiri afya ya mwili

Magonjwa ya fizi na meno ni chanzo kikuu cha kupoteza meno kwa watu wenye umri mkubwa/watu wazima na pia magonjwa haya huhusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke).

Ikiwa magonjwa haya ya fizi yatatambuliwa mapema yanatibika vizuri na kuepusha madhara zaidi.
 
3- Uchunguzi wa kinywa na kusafisha meno kitaalamu ni tiba muhimu zaidi

Ni wangapi kati yetu wenye desturi ya kumwona daktari wa meno walau mara mbili kwa mwaka (walau kila baada ya miezi sita)? Mara nyingi wengi wetu huhangaika na foleni za kumwona daktari wa meno pale tu tunaposumbuliwa na maumivu ama ya jino au kidonda kinywani au kwa sababu ya hali zinginezo zinatotulazimisha kumwona daktari wa meno.
 
Kusubiri mpaka tusukumwe na maumivu ya meno/kidonda kinywani ama ajali yoyote kunatunyima fursa bora zaidi ya kuchunguzwa afya ya kinywa na meno na kusafishwa meno ili kuepusha madhara ya magonjwa ya kinywa na meno kabla hayajatokea ama kukomaa.
 
4- Kupiga mswaki mara mbili kwa siku huepusha kuoza kwa meno

Kupiga mswaki kwa ufanisi walau mara mbili kwa siku huondoa ukoko unaogandiana kinywani na kusababisha kuoza kwa meno. Ukoko huu ni ute laini unaoganda kwenye sehemu mbalimbali za jino/meno huku ukiwa na mamilioni ya vimelea vya magonjwa (bakteria). Matumizi ya nyuzi-safishi kila siku husaidia kuondosha ukoko maeneo ambako mswaki haufiki, vilevile kuondosha ukoko huu kunasaidia kujikinga na magonjwa ya fizi.
 
5- Magonjwa ya kinywa na meno husababisha harufu mbaya mdomoni

Takriban asilimia 85 ya watu wenye harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya kinywa na meno, ikiwa harufu mbaya kinywani inasababishwa na magonjwa kinywani. Dawa za kusafisha kinywa haziwezi kuondoa tatizo zaidi ya kulifunika kwa muda tu.
 
Back
Top Bottom