Nakusimulia kilichotokea jana, najua nae mhusika ataona maana alinielewa jinsi inavyofaa kuishi.
Nilivyo fika Chalinze nikaona nitafute abiria hata mmoja wa kuwa nae maana sikuwa vizuri.Nikafungua uzi wetu,ndani ya dakika mbili tu nikaona uzi umechangamka sana,wazo likanijia nitafute abiria mwenye leseni.
Mungu mkubwa nikampata,akalipa 5,000 kwa madalali mimi nikasema hapana ila tutaendesha wote.
Basi, nikamuachia usukani nikawa namwaga milaiki huku nacheka.Baadae sana tupo mikumi hata story hatuna,ikabidi aniulize upo grupu gani hilo? Nikamuambia jf,akauliza uzi gani? Nikashtuka kidogo,akaniwahi kuwa na yeye ni memba na kwa ukarimu niliomuonyesha akataja na ID yake... Jamani!!!zile lugha za kule na yeye tofauti kabisa... Nikamshauri abadilike,aishi kwa uhalisia tu,ni muelewa na muonekano mzuri tu.Next wiki narudi nae jijini kuuza maparachichi na bamia[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]