Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ugali wa dona ni ugali unaotokana na mahindi ambayo hayajakobolewa katika mashine za nafaka, Kumekuwa na mawazo mgando miongoni mwetu ya kwamba aina hii ya ugali uliwa zaidi na watu wa jamii fulani hususani katika maeneo ya vijijini na makabila fulani.

Ukweli ni kwamba ugali huu unaweza kuliwa na watu wa jamii tofauti bila kuzingatia kabila au jamii ya watu wa vijijini bali ugali wa dona unaweza kuliwa na watu wote kutokana na uwepo wa virutubisho vyote muhimu ambavyo usahidia katika kuongeza nguvu mwilini mwa binadamu.
 
Ulaji wa ugali wa dona ni mdogo sana katika jamii nyingi za Kitanzania, ikilinganishwa na ulaji wa ugali wa sembe unaotokana na unga wa mahindi yaliyokobolewa kwa kisingizio kuwa ugali wa dona unakosa radha tofauti na ugali wa sembe.

Wakati jamii nyingi ya Watanzania wakiwa na mtazamo huo kuhusu ugali wa dona, baadhi ya wataalam wa kilimo na vyakula, wanasema mbali na ubora wa kiafya wa ugali huo wa dona kutokana na kuwa na virutubisho vingi vinavyohitajika mwilini ukilinganishwa na ugali wa sembe, kusaga mahindi bila ya kuyakoboa kunamfanya mlaji kupata unga mwingi zaidi.
 
Kwa mujibu wa wataalam hao, ukoboaji wa mahindi unapoteza kiasi kikubwa cha unga pamoja na virutubisho vingi vinavyopatikana kwenye zao la mahindi, kama vile mafuta, protini, madini, vitamin na nyuzinyuzi (fibre), vitu ambavyo vinaelezwa kusaidia kuimarisha zaidi lishe ya mlaji.

Kwa mujibu wa Mchambuzi wa Sera kutoka Taasisi ya Utafiti nchini ya REPOA, Godfrey Bwana, amesema kuna upotevu mkubwa wa chakula nchini unatokea wakati wa maandali ya chakula husika, hasa vyakula aina ya nafaka ambapo alifafanua kuwa kati ya asilimia 10 na 40, hupotea kila mwaka wakati wa maandalizi hayo ya vyakula, hasa ukoboaji.
 
Rais wa Shirikisho la Muungano wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania, Profesa Joyce Kinabo kutoka Chuo cha Kilimo Morogoro (SUA) alifafanua umuhimu wa lishe sanjari na vyakula vya asili ni kwamba nchi za Afrika bado hazijafanya vyema katika masuala ya lishe licha ya jitihada mbalimbali kuchukuliwa lakini bado kuna changamoto kubwa ya tafiti zitakazowezesha wataalamu wa lishe kupata taarifa sahihi ili kudhibiti suala hilo.
 
Aidha aliwahimiza wananchi kula vyakula mbalimbali vya asili kama vile Ugali wa mahindi ambayo hayajakobolewa (dona) ambao aliutaja kuwa na virutubisho vyote muhimu kwa kuwa mahindi yake ayafanyiwi mchakato wowote katika maandalizi yake hivyo ubaki na ubaora wake kwa kuwepo na virutubisho vyote muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…