Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mlo wenye mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubishi vya aina zote, huitwa “mlo kamili”. Mlo kamili ni muhimu sana hasa kwa watoto, ambao huwasaidia kukua vizuri na kuwa na afya njema. Mlo kamili humwezesha mtu kujikinga na madhara ya maradhi mbali mbali kama vile malaria, surua, kuharisha, shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo na hata ukimwi.
 
Mgawanyo wa vyakula

· Vyakula vyenye wanga
Hivi ni muhimu katika kuupa nguvu mwili za kufanya kazi mbali mbali. Vyakula vyenye wanga ni pamoja na: nafaka, kama mahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi, uwele na kadhalika. Wanga pia hupatikana katika mihogo, viazi vitamu, viazi ulaya, viazi vikuu, magimbi, ndizi, miwa na asali.
 
· Vyakula vyenye protini
Protini ni muhimu sana katika kujenga mwili na kuwezesha ukuaji wa mwili hasa kwa watoto na pia husaidia kutengeneza kinga ya mwili. Vyakula vyenye protini ni pamoja na: nyama, (ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata, samaki, mayai, maziwa na kunde, maharage, soya, dengu, choroko, njegere, mbaazi, na njugu mawe.
 
· Vyakula vyenye mafuta
Vyakula vyenye mafuta huleta joto mwilini, na vile vile huleta nguvu mwilini na kulinda na kulainisha ngozi na pia utando (membrane). Mafuta hutokana na mimea na huwa yanauzwa madukani kama vile, mafuta ya karanga, alizeti, nazi, ufuta, korosho, mawese, mbegu za maboga, mbegu za pamba.
 
· Matunda na mboga mboga
Matunda na mboga mboga ni muhimu sana katika mwili, kwa vile vyakula hivi vina vitamini na madini mbali mbali ambayo ni muhimu mwilini. Vitamini na madini huhitajika kwa kiwango kidogo sana lakini ni muhimu kwa mwili kuweza kufanya kazi zake vizuri. Upungufu wa vitamini na madini mwilini unaweza kusababisha hitilafu mbali mbali katika mwili na hata kusababisha kasoro zinazoambatana na maradhi mwilini.
 
Madini ya chuma hupatikana katika nyama,( ng’ombe, nguruwe, kondoo), mboga za majani kama mchicha.

· Madini ya chokaa (Calcium)
Hutumika katika utengenezaji wa mifupa na meno imara. Husaidia ugandaji wa damu, kama mtu ana jeraha ili kuzuia damu kuendelea kuvuja, na pia ni muhimu katika chembe chembe za mishipa ya fahamu. Madini ya chokaa hupatikana katika maziwa na mboga za majani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…