Kuhisi njaa. (Watu wengi hudhani kuhisi njaa ni dalili ya kutakiwa kula chakula, lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine kuhisi ni dalili ya kutakiwa kunywa maji.)
Swali la kujiuliza ni, je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (250ml) sawa na lita 2 kwa siku.
Swali la kujiuliza ni, je unatakiwa kunywa maji kiasi gani kwa siku? Wataalamu wa afya wanashauri unywe maji angalau glasi 8 (250ml) sawa na lita 2 kwa siku.
Baada ya kujua dalili za ukosefu wa maji mwilini pamoja na matatizo utakayopata kama hutokunywa maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili wako. Napenda ujijengee hizi tabia nzuri za kiafya wakati unapohitaji kunywa maji…
Kila unapotaka kula, kunywa maji kabla ya kuanza kula chakula chako. Vilevile kunywa maji wakati ukiendelea kula na mwisho wa kula chakula kunywa maji tena.
Hakikisha unajijengea tabia nilizozitaja hapo juu, ni rahisi ukishapata mazoea ya kufanya hivyo kila unapotaka kunywa maji. Kwa kuwa maji ni muhimu na yanakazi nyingi sana mwilini, zifuatazo ni faida za maji mwilini kiafya.
1. Maji husaidia kuboresha ngozi.
-Seli za ngozi zinahitaji maji kwaajili ya kazi zake zikiwemo kulinda ngozi kwa kupambana na magonwa mbalimbali yakiwemo eczema, psoriasis na hata makunyanzi na kukauka kwa ngozi. Hivyo ukitaka kuoenekana mwenye ngozi nzuri kama ya mtoto penda kunywa maji kwa kiwango kinachotosha.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.