Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Leo nimeenda mgahawani nikakuta kila meza watu wamekaaa wawili wawili(couple) .. kwakua sipendi kula nikiwa nimesimama
Nikachukua simu yangu nikapiga nikaongea kwa sauti rafiki yangu mke wako yuko hpa mgahawani amekaa na mwanaume mwngine njoo uone...
Robo tatu ya wanawake waliokua hapa wameondoka meza zimebaki waz nadhani wanaenda kula nyumbani
 
Jamaa kakichukua cheti cha ndoa na kukitizama kwa muda mrefu kila mkewe akiingia chumbani anamkuta jamaa kakikodolea macho takriban masaa matano kitu ambacho si kawaida mkewe kamuangalia mwisho kamuuliza unaangalia tarehe yetu tuliofunga ndoa? Jamaa huku akisonya na kukitupa cheti kitandani huku akisema "sijui kwanini huwa hawaandiki expire date!
 
HABARI NJEMA KWA WATUMISHI WA UMMA KUHUSU MADARAJA!

SERIKALI imetoa ufafanuzi RASMI kuhusu MADARAJA hii LEO. Kwa kuzingatia hali halisi ya nchi yetu na ukuaji wa uchumi pamoja na kuimarika kwa shilingi dhidi ya DOLA YA MAREKANI, Serikali inapenda kutoa ufafanuzi MADARAJA kama ifutavyo:

1. Daraja la Mkapa - lipo Mto Rufiji kupitia KIBITI.

2. Daraja la Kikwete - Lipo Mto Malagarasi huko Kigoma.

3. Daraja la Mwl Nyerere - lipo Bahari ya Hindi, unavuka kwenda Wilaya mpya ya Kigamboni.


Watumishi wa Umma mnashauriwa kuwa wastahimilivu mnapovuka madaraja hayo ambayo ni viashiria vya maendeleo ya nchi yetu kwani mengine ni marefu sana!!!
 
dah jmn kumbe kwenda kanisani raha sana

*Jana nimeenda church pasta akasema mgeukie jirani yako mwambie deni langu limelipwa na Yesu*

*ile nageuka tu nakutana na baba mwenye nyumba bas nikaongeza sauti ili asikie vizuri*


sasaivi katoka nje sijui kaenda kuniandikia risiti
 
Nakusihi mwanaume ufanye kazi ili umletee chakula mke na c yeye akuletee chakula. Kumbuka kwa mara ya kwanza mwanamke kumletea chakula mwanaume ilikuwa ni pale Eden na tulijikuta tumefukuzwa wote Bustani ya Eden... Usisubir kufukuzwa hapo Ulipo

Chakula cha kuletewa na mwanamke hakitakuacha salama
 
Sisi Wenye Vidole Kama Chanuo la Mbao Tunasumbuliwa Sana Na Sim za Smartphones

Mama Mkwe Katuma Sms Kutusalimia Nikamjibu (KWEMA HUKO MAMA ?).. Baada Ya Kusend Nkaikuta Imejiandika (KWENDA HUKO MAMA).

Sasa Hivi Kila Nikimpigia Hapokei!!

NAFANYAJE HAPA SASA JAMANI
 
Sisi Wenye Vidole Kama Chanuo la Mbao Tunasumbuliwa Sana Na Sim za Smartphones

Mama Mkwe Katuma Sms Kutusalimia Nikamjibu (KWEMA HUKO MAMA ?).. Baada Ya Kusend Nkaikuta Imejiandika (KWENDA HUKO MAMA).

Sasa Hivi Kila Nikimpigia Hapokei!!

NAFANYAJE HAPA SASA JAMANI
Dah
Pole sana ila nenda pale veta chang'ombe watakusaidia kuiweka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom