Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

a5976f4df2dd1cf64762a3cdada9a767.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shuka au blanketi ni moja ya nguo muhimu zinazotumika kila siku. Tofauti ni kwamba hazionekani hovyo. Zipo chumbani ambako usafi wake unaendelea kuwa tofauti na nyingine kama gauni, suruali.
 
“Sijawahi kulifua blanketi langu kwa muda wote niliolitumia nikiwa chuo kikuu,” anasema Jonathan Abel, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma. “Nilikuwa silitumii mara nyingi,” anajitetea.

Shuka au blanketi ni moja ya nguo muhimu zinazotumika kila siku. Tofauti ni kwamba hazionekani hovyo. Zipo chumbani ambako usafi wake unaendelea kuwa tofauti na nyingine kama gauni, suruali.
 
Jonathan anasema baada ya kujiunga na chuo hicho hakujua kama Dodoma kuna baridi. Ilikuwa mara yake ya kwanza kufika mji huo, makao makuu ya Tanzania akitokea Bukoba.

Nilipoenda likizo kubwa nilirudi na blanketi la kilo tano. “Sikulifua mpaka namaliza chuo. Lilikuwa zito linalohitaji mashine kulisafisha,” anakumbuka. Siyo Jonathan peke yake, vijana wengi hawakumbuki usafi wa shuka au blanketi.
 
Wanafunzi wa ngazi zote, makondakta, wanamichezo pia na pengine wanaume wasiioa kwa ujumla. Ni nadra kwao kukumbuka kufua nguo hizi.

Tafiti

Kuna vitu vitatu vinavyochangia kutozingatia usafi wa nguo hizi. Umri, jinsia na ndoa. Utafiti uliofanywa Agosti mwaka 2014 na YouGov ya Uingereza ulibaini vijana, chini ya miaka 24 hawafui mashuka wakilinganishwa na wazee wenye zaidi ya miaka 60.
 
Majibu ya utafiti huo yalisema, linapojadiliwa suala la usafi wa kitanda, Waingereza wamegawanyika kwenye makundi matatu. Wale wafuao kila wiki, kila baada ya wiki mbili na wale wanaofua zaidi ya kila wiki tatu.
 
Theluthi moja, kwa mujibu wa utafiti huo, wanafua kila wiki. Lilifuatiwa na asilimia 35 ya wanaofua kila baada ya wiki mbili. Hili ndilo lilikuwa kundi kubwa zaidi. Asilimia nane wanafua kila baada ya wiki tatu na mmoja kati ya watu 10 walifua kila baada ya wiki nne. Asilimia nne wanafua kila baada tano na kuendelea wakitofautiana na asilimia tatu wanaofua zaidi ya mara moja kwa wiki.
 
Utafiti huo uliohusisha washiriki 1,866 wenye umri kuanzia miaka 18 ulibaini wanaume ni wavivu zaidi kwenye suala hilo. Wanaume wengi walisema shuka au blanketi huchafuka baada ya kutumika kwa walau wiki nne wakati wanawake walisema ni wiki tatu.
 
Utafiti huo uliohusisha washiriki 1,866 wenye umri kuanzia miaka 18 ulibaini wanaume ni wavivu zaidi kwenye suala hilo. Wanaume wengi walisema shuka au blanketi huchafuka baada ya kutumika kwa walau wiki nne wakati wanawake walisema ni wiki tatu.
 
Wanawake pia walisema hawawezi kuendelea kutumia mashuka baada ya wiki tatu wakati wanaume walisema hata baada ya wiki sita bado wangeweza kutumia. Kwa ujumla, nusu ya washiriki walisema wanapata shida kutumia shuka baada ya kuitumia kati ya wiki mbili mpaka tatu.
 
Amina Hussein anasema usafi wa shuka ni kitu anachokipa kipaumbele. “Mchana huwa natandika shuka jeupe…likianza kupata uchafu najua tayari, hata nalojifunika nalo ni chafu,” anasema ingawa anasema hajui huwa anafua kila baada ya muda gani.
 
Mpaka nione yamebaki machache kabatini ndiyo nafua. Hiyo ni kazi ya wikendi nzima na nikifanya hivyo naweza nikamaliza hata miezi miwili au mitatu,” anasema.

Utafiti uliofanywa na kampuni ya magodoro Uingereza, Ergoflex, mwaka 2013,
 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Marina Njerekela anashauri kubadilisha mashuka mara kwa mara kulingana na matumizi ya mtu kwani uchafu unaoweza kuwapo huenda ukasababisha madhara kwa afya ya binadamu anayeyatumia.
 
Back
Top Bottom