Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

mbali na magonjwa kuna wadudu mfano viroboto na kunguni ambao huishi sehemu chafu ikiwamo mashuka na magodoro ni moja ya wanazojificha hivyo ni jambo jema kuchukua tahadhari kabla madhara kama kutokwa upele na muwasho hayajajitokeza.

Uchafu

Wataalamu wa afya wanatahadharisha juu ya vyanzo tofauti vya uchafu unaoweza kuwamo kwenye shuka au blanketi.
 
Ipo tofauti ndogo kati ya maeneo yenye baridi mfano kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini na yale ufukweni mwa bahari; Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ambayo yanakuwa na joto.

Wanasema, kila ulalapo, kuna mamilioni ya bakteria ambao huwezi kuwaona kwa macho watokanao na mabaki ya vyakula, vumbi, fangasi na uchafu wa chavua za maua.
 
Majira ya joto; joto na takamwili nyinginezo na vyanzo vya uchafu kwa mashuka na mablanketi.

Mafuta na vipodozi vinginevyo, uchafu wa miguu na ngozi unaobaki kwenye mashuka unaweza kusababisha muwasho, mzio na ukizidi, maambukizi. Pia wadudu; mende, kunguni na viroboto hupenda kujificha kwenye chaga za kitanda au mifumbati yake.
 
Utafiti uliofanywa mapema mwaka huu na Journal of Medical Entomology la Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza unaeleza, kunguni wanavutiwa zaidi na mashuka mekundu.

“Tulikuwa tunatafuta namna mpya ya kukabiliana na kunguni,” alisema Dk Corraine McNeill, kiongozi wa utafiti huo na kuongeza: “Kunguni wana rangi wanayoipenda kuliko nyingine. Nyekundu.”
 
Ushauri

Dk Njelekela anashauri ujenzi wa nyumba imara ambazo zitazuia vumbi kuingia ndani kwa urahisi na kuchafua mashuka na godoro ndani ya muda mfupi. Anasema: “Vyumba visivyoruhusu hewa ya kutosha vinaweza kusababisha magonjwa ya koo na kifua kutokana na vumbi litakalojilimbikiza kwenye mashuka.”
 
Ushauri

Dk Njelekela anashauri ujenzi wa nyumba imara ambazo zitazuia vumbi kuingia ndani kwa urahisi na kuchafua mashuka na godoro ndani ya muda mfupi. Anasema: “Vyumba visivyoruhusu hewa ya kutosha vinaweza kusababisha magonjwa ya koo na kifua kutokana na vumbi litakalojilimbikiza kwenye mashuka.”
 
Anasema kuwa hali kama hii inajidhihirisha zaidi vijijini ambako nyumba nyingi hazina madirisha makubwa kuweza kupitisha hewa ya kutosha hali inayosababisha vumbi kuzagaa mpaka vyumba vya kulala.

Dk Eliza Wampembe wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili (Muhas), anasema magonjwa yakuambukiza kama fangasi na mapunye huweza kuenezwa kutokana na kuchangia mashuka, hivyo kuwakanya wanafunzi wenye tabia ya kubadilishana mashuka au kulala pamoja.
 
Watoto wadogo wapo kwenye hatari zaidi. Wazazi wanatakiwa kuwa makini na kutowalaza watoto wao sehemu ambao zimelaliwa na watoto au watu wengine bila kubadilisha mashuka,” anasema Dk Eliza.

Anashauri kufua shuka mara nyingi iwezekanavyo na kulianika juani na ikiwezekana, kupiga pasi ili kuua vijidudu vinavyoweza kuwamo.

Anakumbusha: “Ukijali afya yako utakuwa imara na utaweza kutimiza ndoto zako kwani mawazo mazuri ya baadaye huletwa na hisia nzuri na mwanana ukiwa usingizini.’
 
IMG-20170813-WA0002.jpg
dk 8 tayari jamaa amesharudi wavuni
 
Back
Top Bottom