Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. Nguo zenye madoa, kabla ya kutumia dawa ya madoa jaribu kwanza kutoa madoa kwa kutumia sabuni ya unga aina ya "OMO". Jamani kwenye ukweli usemwe, hii sabuni ni kiboko ya madoa. Fua kwanza nguo yenye dowa itakate kabisa, kisha isuuze vizuri , halafu weka maji masafi kwenye beseni, weka sabuni ya omo, changanya itoe povu kisha loweka nguo yako yenye doa kwa masaa kadhaa, kama matatu hivyi kabla hujaifua kwa mara ya pili, msisitizo ukiwa kwenye eneo lenye doa. Nguo zenye madoa ndio ziwe za kwanza kuanza kufua, ziloweke mapema asabuhi,
 
fanya shuguli zako, unapoanza kufua unazifua za kwanza sabuni itakuwa imepata muda wa kupenya kwenye doa na kuondoa doa.Dowa likiwa kali na limeshindikana kutolewa na omo basi weka dawa ya madoa, mfani JIKI, ila kuwa makini kuna jiki kwa ajili ya nguo za rangi na kuna jiki ya nguo nyeupe. Tumia jiki sahihi ili kuepuka kuharibu nguo.
 
Vitu vya kuzingatia:
1. Nguo isuuzwe zaidi ya mara moja ili kuondoa sabuni yote kwenye nguo
2. Nguo inapo anikwa ikungutwe ili kupunguza mikuchamano, na kisha igeuzwe ndani nje ili kuzuia kupaushwa na jua
3. Nguo isishinde kwenye kamba kutwa nzima, ikikauka tu itolewe, ikunjwe na kuhifadhiwa vizuri.
4. Nguo isilowekwe ikiwa chafu(bila kufuliwa kwanza ikatakata), hii inasaidia nguo isifubae kwa kufyonza uchafu.
 
5.Tumia sabuni nzuri ambayo haita haribu mikono yako.
6.Tumia sabuni sahihi kuna sabuni kwa ajili ya nguo za rangi na kuna sabuni kwa ajili ya nguo nyeupe. Sabuni zilizo undwa kwa ajili ya nguo nyeupe zinawekwa dawa ya madowa, ukitumia kwenye nguo za rangi nguo zako zinakuwa zinapauka taratibu taratibu kila zinapo fuliwa.
7. Tumia vibanio ili kuhakikisha nguo zako hazianguki na kuchafuka, ukajikuta unarudia zoezi la kufua kwa mara ya pili.
 
8. Vibanio vya kuanikia nguo vihifadhiwe kwenye container safi lenye mfuniko, baada ya kuanua nguo, toa vibanio kwenye kamba vihifadhi vizuri kwenye container lake.Usiache vibanio kwenye kamba, vinaharibiwa na jua, baada ya muda vitapasuka.
9.Nguo zinazotoa rangi zianikwe mbali na nguo zingine, yaani kila nguo isigusane na ingine, zipeane nafasi ya kutosha kwenye kamba kuzuia kuvujiana rangi.
 
Kila jambo hapa duniani lina kanuni na taratibu , basi tuzingatie kanuni za kutunza na kufua nguo, tufundishe watoto wetu na wadogo zetu, ili wasije kuwa kama mtu yule aliye sema "I always wear gloves when I wash my hands", maana wakifanya hivyo aibu itakuwa kwetu sisi tulio walea bila kuwajuza. TAFAKARI kisha chukua hatua.
 
Back
Top Bottom