Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. Hatua ya kwanza ukisha chukua nguo zako chafu namna hiyo ni kuziweka katika mafungu mafungu kabla ya kuanza kuosha. Nguo nyeupe zinakaa fungu lake, nguo zenye rangi nyeusi, dark blue, dark brown, dark grey etc(yani dark colours) na zenyewe fungu lake. Nguo ambazo ni chafu sana, au nguo delicate mfano gauni la lace material (lace dress), au nguo zinazotoa rangi ,
 
IMG-20170813-WA0035.jpg
 
2. Chukua beseni zako za kufulia weka maji masafi, beseni moja ni la kufulia, jingine la ku suuzia. Weka sabuni yako ya unga kwenye beseni la kufulia, kisha ichanganye kwa mkono mpaka itoe povu, halafu dumbukiza nguo zako na kisha anza kufua. wakati wa kufua unazingatia maeneo ya kola, makwapa, kama ni kanga kwenye pindo, kama nguo ina mifuko, basi kwenye mifuko, na pia kwenye pindo za suruali. unapaka sabuni ya kipande kwenye hayo maeneo na kusugua vizuri. kisha unaishika nguo kama unaitandaza na kuisugua randomly kila upande.
 
3. Nguo nyeupe unatumia maji yasiyokuwa na vumbi, itakuwa vyema zaidi kama utatumia maji yaliyo tuliya, labda yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye ndoo au pipa na hivyo vumbi kutuwama chini. Mimina maji hayo taratibu kwenye beseni la kufulia na la kusuuzia. Weka sabuni changanya kwa mkono , weka nguo zako nyeupe fua kama ulivyo fua za rangi. Kama unaweza pata maji ya uvuguvungu huwa ni mazuri kwa kufulia nguo nyeupe.
 
Back
Top Bottom