Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

22dbd3caff37640f488b25a221ce9e9a.jpg
 
Utafiti uliofanywa mapema mwaka huu na Journal of Medical Entomology la Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza unaeleza, kunguni wanavutiwa zaidi na mashuka mekundu.

“Tulikuwa tunatafuta namna mpya ya kukabiliana na kunguni,” alisema Dk Corraine McNeill, kiongozi wa utafiti huo na kuongeza: “Kunguni wana rangi wanayoipenda kuliko nyingine. Nyekundu.”
 
Ushauri

Dk Njelekela anashauri ujenzi wa nyumba imara ambazo zitazuia vumbi kuingia ndani kwa urahisi na kuchafua mashuka na godoro ndani ya muda mfupi. Anasema: “Vyumba visivyoruhusu hewa ya kutosha vinaweza kusababisha magonjwa ya koo na kifua kutokana na vumbi litakalojilimbikiza kwenye mashuka.”
 
Anasema kuwa hali kama hii inajidhihirisha zaidi vijijini ambako nyumba nyingi hazina madirisha makubwa kuweza kupitisha hewa ya kutosha hali inayosababisha vumbi kuzagaa mpaka vyumba vya kulala.

Dk Eliza Wampembe wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili (Muhas), anasema magonjwa yakuambukiza kama fangasi na mapunye huweza kuenezwa kutokana na kuchangia mashuka, hivyo kuwakanya wanafunzi wenye tabia ya kubadilishana mashuka au kulala pamoja.
 
Watoto wadogo wapo kwenye hatari zaidi. Wazazi wanatakiwa kuwa makini na kutowalaza watoto wao sehemu ambao zimelaliwa na watoto au watu wengine bila kubadilisha mashuka,” anasema Dk Eliza.

Anashauri kufua shuka mara nyingi iwezekanavyo na kulianika juani na ikiwezekana, kupiga pasi ili kuua vijidudu vinavyoweza kuwamo.

Anakumbusha: “Ukijali afya yako utakuwa imara na utaweza kutimiza ndoto zako kwani mawazo mazuri ya baadaye huletwa na hisia nzuri na mwanana ukiwa usingizini.’
 
Back
Top Bottom