Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, anasema kuwa kunywa maji ni muhimu yawe baridi au ya moto na hakuna sababu za kitaalamu zinazohusisha na dawa au kutibu kitu chochote.
Anasema, watu wa tiba mbadala ndiyo wamelikuza hilo lakini kitaalamu halipo na kunywa maji ni muhimu kwa kila mtu bila kujali ni ya moto au baridi, hayo mengine ni maneno tu.