Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usafi huu unamwepusha na uwezekano kuambukizwa magonjwa na kupata athari za kikemikali zinazotokana na kemikali,vikolezo na sumu nyingine zinazoleta magonjwa.

Usafi ndiyo unaoondoa majitaka, vumbi, marundo ya taka ngumu, vichaka vinavyozunguka mitaa na makazi na kelele za mashine mbalimbali.
 
Teknolojia ni muhimu kwani ndiyo inayorahisisha kufanya kazi za kukabiliana na uchafu kama kujenga vyoo, mitaro ya maji taka, mashine zinazotumika kusafisha na kuzoa taka, kusambaza maji na huduma za kuosha mikono kwa sabuni baada ya usafi au kutumia vyoo vya nyumbani na umma.
 
Usafi unatakiwa kuanzia ndani kabla hatujaangalia mazingira yanayotuzunguka, leo sizungumzii usafi wa ndani ya nyumba zetu mathalani ndani ya jiko, vyumbani, sebuleni na vyooni , nazungumzia nje kwenye viwanja vinavyotuzunguka.

Ni ajabu kuwa ule utamaduni wa kusafisha kila siku eneo la nje ya nyumba iwe mijni au vijijini umeanza kutoweka tofauti na zama hizo ambapo kazi zilifanyika asubuhi na jioni . Kila eneo utakalopita mjini na vijijini utakutana na watu wakiwa wameshikilia mifagio wakisafisha nje ya eneo ya nyumba wanazoishi.
 
Hali hiyo ilikuwa inavutia kutokana na kudumisha usafi ulioondoa vipande vya karatasi, mabaki ya vyakula, hata vinyesi vya wanyama na ndege kama kuku na bata, lakini tofauti na ilivyokuwa hivi sasa mazingira ya nyumba nyingi hayasafishwi.

Yawezekana zikapita siku tatu au wiki eneo la nje halijaguswa, kuna magunzi, karatasi, mifuko ya nailoni, vifuu na majani yanayodondoka juu ya miti.
 
Kupotea kwa utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira ni sababu kuu ya taka kulundikana na wakati mwingine kuwa chanzo cha maradhi kama malaria, kuhara na kutapika.

Bila kujali wapi ulipo, usafi wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya watu wote iwe ni katika miji na vijijini, ndiyo unawaepusha watu na magonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…