Kwa mfano, nje ya nyumba kukiwa kumezagaa takataka kunaonekana vibaya, kama kuna nyasi ndefu haipendezi, kukiwa na maji machafu ndiyo mazalia ya mbu, inzi, konokono na vyura.
Takataka hizo zikiachwa kurundikana kwenye njia za kuingilia ndani ya nyumba au kwenye vijia vya karibu ya nyumba ni kero na aibu.
Nyakati nyingine , mikebe, vyombo vya plasitiki kama chupa na vifungashio hata karatasi na mifuko ya nailoni huachwa nje ya nyumba na kuzagaa kila mahali. Hivi vinaweza kuwa makao ya wanyama na wadudu waharibifu kuanzia nyoka, panya, mbu na mende.