Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utafiti unaonyesha kuwa kiwango cha mmeng'enyo na sukari kwenye damu kinapungua kama wanga ikipikwa na kuliwa kama kiporo (baridi), lakini hupunguza zaidi kiwango cha sukari kwa asililia 50% kama ikiwa kiporo na kupashwa moto.
Hii ni kutokana na virutubisho vingi kutomeng'enyeka kirahisi baada ya wanga kupoa na kupashwa moto.
 
Utafiti huu ulifanywa kwa kutumia tambi, lakini hii ni tabi aya vyakula vingi aina ya wanga.
Hii inamaanisha nini kwako wewe mlaji? Utafiti huu unatoa ufafanuzi mzuri juu ya vyakula tunavyokula.
Kutokana na matokeo haya, ni vizuri zaidi kula na kushiba kiporo cha jamii ya wanga sababu hakitokufanya uongezeke uzito kama utakapokula chakula cha kawaida.
 
Hii ni kwa sababu nusu ya chakula unachokula ndio kinachotumika kukupa karoli mwilini na kilichobaki huishia kutoka kama makapi.
Watu wengi sana wanapenda kupunguza uzito bila kuvuruga kula, hii inawezekana kama utafanya mazoezi magumu na ya muda mrefu.
 
Lakini kwa kupata matokeo mazuri zaidi, kupunguza kula vyakula visivyo na afya ni kitu muhimu zaidi kuliko hata mazoezi.
Nasema hivi sababu chakula ndio kinachokufanya uongezeke uzito, lakini si swala la kujinyima kula, ni swala la kujua jinsi ya kula vyakula visivyokufanya unenepe.
Vyakula vya kuzuia ni chumvi, sukari, na mafuta yasiyo na afya kama yalivyoelezewa hapa. Lakini leo unaongeza kiporo kwenye orodha ya vyakula vya kula bila kuwa na wasiwasi wa kunenepa.
 
Unaweza kuwa na swali, je kwanini ukila kiporo huwa nahisi kuvimbiwa na tumbo kujaa? Jibu ni rahisi, na sababu pekee ni kuwa unakosea kupasha moto kiporo chako, na jibu liko hapa chini. Lakini kwanza tuangalie jinsi ya kuhifadhi kiporo.
Je unahifadhi vipi kiporo ?
 
Ili kuzuia madhara ya kula chakula kisicho bora, kuwa makini kwenye kuhifadhi chakula vizuri.
Ili kuhifadhi chakula chochote ni lazima kukiweka kwenye mazingira yanayozuia wadudu kuzaliana.
Hivyo basi, ili kulinda chakula muda mrefu na kuepukana na madhara ya kuingiwa na vijidudu vinavyoweza kuleta sumu, weka chakula kwenye jokofu mara tu baada ya kumaliza kula.
 
Vyakula vingi huharibika haraka na kuingiwa na wadudu mara tu vikishapoa, hasa vyakula vyenye protini ambavyo huharibika haraka sana vikihifadhiwa vibaya.
Ni vizuri kulinda afya yako kwa kuhakikisha chakula kimehifadhiwa vizuri ili kuweza kuliwa wakati kinapohitajika.
Jinsi ya kupasha moto kiporo
 
Je unapasha moto vizuri kiporo chako? Inawezekana ukaona ni swali lisilo na msingi, lakini mara nyingi wengi wetu hatufahamu jinsi ya kupasha moto kiporo.
Wengi huweka jikoni na kuwa na papara ya kula kabla hakijapata moto vizuri. Hii si sawa, sababu kila chakula huwa na masharti yake kwenye kupasha moto.
Moto husaidia kuamsha
 
virutubisho na vilevile kuua vijidudu vilivyozaliana kwenye chakula.
Ukiwa unapasha moto kiporo cha wali, ni vizuri ukakiweka jikoni muda mrfu ili kipate moto vizuri.
Hii ni muhimu sana, siyo tu kuua vijidudu, bali hukuwezesha kupata urahisi kwenye kukisaga chakula tumboni.
 
Back
Top Bottom