Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pole kuhusu afya ya mzazi. Mungu ndiye tabibu mkuu na bila shaka Atamgusa na mkono wake wa uponyaji. Mamangu pia hali yake siyo nzuri na usinione niko hapa ni kujifariji tu. Yote tumwachie Mungu rafiki yangu. Wazazi wetu hawa ni wazee na kusema kweli tumebarikiwa sana kuachiwa tukawa nao mpaka wakati huu. Ni mapenzi na upendeleo wa aina yake na hatupaswi kulalamika. Wakati huu wanapokuwa ukingoni mwa maisha yao kizazi chao kikiondoka baada ya kutimiza majukumu yake tena kwa ustadi wa ajabu na kupisha vizazi vingine, tujaribu kuwa karibu nao na kung'ong'a ng'ong'a matone ya mwisho katika bahari yao pana ya maarifa, hekima na uzoefu wao kuhusu maisha. Mungu Atubariki na kututia nguvu mkuu...
 
Na kila zito(tatizo) au jepesi(furaha) mshirikishe mwenzi wako.Mke/mume lazima awe rafiki yako zaidi ya kuwa mume na mke... Kila siku iendayo kwa Mungu peaneni ubuyu mpya,hata kama ni wa insta au Facebook.Jitahidini kukumbushana jinsi mlivyo kutana kwa mara ya kwanza na jinsi mlivyo sumbuana,lakini pia,tembeleeni ile g/house mliyo duana kwa mara ya kwanza.
ZINGATIA:Vinywa vyenu msiviruhusu vitoe maneno ya matusi,dharau,kebehi,n.k. dhidi yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…