Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili
Kwa wale wenye matatizo ya uzito wa mwili ambao wakati mwingine unaweza kuwa hatari kwa afya, kwa kusababisha matatizo kama Presha, kisukari na magonjwa ya moyo, maji yanaweza kuwa kimbilio lako. Kwa mujibu wa utafiti , watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa siku yaani angalau glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya na wakati wa kula wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako kupata chakula kile kile kinachohitajika na hivyo kuondoa uwezekano wa mwili wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako uendelee.