Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku moja mfalme huyo aliwaamuru watu wenye busara wamtafute mtu mwenye furaha katika milki yake ili amuone atakuwa wa namna gani. Walipompata na kumleta mbele yake alistaajabu sana.

Alikuwa mtu wa hali ya chini wala hakuwa na mali. Hata nguo alizovaa zilikuwa zimechakaa mno. Lakini kwa vigezo vyote walihakikisha kuwa pamoja na maisha duni alikuwa mtu mwenye furaha kamili.
 
Hii ni hadithi yenye somo. Tunajifunza kuwa fedha au mali pekee hazitoshi kumfanya mtu kuwa na furaha ambayo kila mmoja wetu anaihitaji. Hii haijalishi hadhi au madaraka kwani hata mtu mwenye wadhifa mkubwa duniani anahitaji furaha ili kuwa na raha ya maisha. Hivyo, hakuna sababu ya kuishi katika huzuni na mashaka.
 
Wakati wowote unapopata taarifa mbaya, moyo hushtuka na kuufanya uende mbio hivyo ili kuurudisha katika hali yake ya kawaida unatakiwa kuvuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu. Hatua hii itasaidia kutuliza mapigo ya moyo.
 
Ukifanikiwa kufanya hivyo, jitahidi kutabasamu mara kwa mara, hata kama ni kufanya hivyo kutokana na aina ya tukio au taarifa ulizonazo. Kutabasamu husaidia kuchangamsha akili. Ingawa inaweza kuchukua muda fulani, wataalamu wanasema inasaidia kuamsha hisia za furaha zilizoshambuliwa na huzuni.
 
Huzuni inapokutokea huyakuta mawazo mengine akilini ambayo huyaondoa. Nafasi hiyo punde huchukuliwa na huzuni. Hali hii ikitokea unashauriwa kujilazimisha kurudisha akilini mawazo ya awali kabla mambo hayajabalika.
 
Lengo likiwa kufufua furaha iliyokuwepo. Ikiwa hutafanikiwa licha ya kufuata hatua hizo zote, wasaidie walio karibu yako kufurahi jambo walilonalo. Kwa mfano, unapokuwa msibani, chukua jukumu la kuwanyamazisha wenzako na kuwapa faraja. Ukifanya hivyo utakuwa umejisaidia kuondokana mawazo yaliyokufanya ulie.
 
Back
Top Bottom