Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Usikate tamaa. Hata Mungu Hapendi. Kama nilivyosema mara ya mwisho, tusisahau mibaraka ya kuwa na hawa wazee wetu mpaka wakati huu. Wengi hawakupata bahati hiyo. Tuendelee kumtegemea Mungu rafiki yangu. Mama yeye ana ka unafuu kidogo. Tatizo lake linahitaji operesheni kubwa na hatari lakini yeye mwenyewe hataki. Hata madaktari wanasema kwamba kulingana na umri wake operesheni hiyo haitakuwa na maana yo yote. Hata leo nimeongea naye kwenye simu. Ameniimbia nyimbo nzuri za utotoni, tukalia na kutakiana mema. Ndiyo maisha ndugu yangu...Mkuu ujio wangu humu ni ili nikutane na ndugu zangu wenye kujua maana ya faraja ni nini. Hakuna unafuu,sijui,labda nakata tamaa mimi,Mungu anipe ujasiri... Sipendi kukuuliza wewe maana naogopa,naangaliaga posts zako,zikiwa za furaha najua mama anaendelea vizuri.Tuwaombee sana..