Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usimuulize mpenzio anataka zawadi gani.Siku zote zawadi ni kitu ambacho mpokeaji hakijui na wala hatakiwi kukijua kabla hujampelekea.Kuna zawadi nyiingi sana ambazo unaweza mpa mwenza.Na kupitia muda wa urafiki wenu naamini utaweza kujua walau nusu kama si robo tatu ya vitu anavyovipenda.Ila jitahidi uwe ni muibuaji wa vitu vipya sio vilivyozoeleka.
 
Natumaini kwa kiasi Fulani vitu kama hivyo kutoka kwa mwenza wako vimekufanya au vinakufanya umpende zaidi.Au ukosaji wa vitu hivi kwa mwenzako vimekufanya mshindwe kuendelea kua katika mahusiano au kuvunjika moyo.Jiheshimu na pia muheshimu mwenzako pamoja na hisia zake,mjali,mthamini,mtie moyo,mrekebishe anapofanya ndivyo sivyo na lingine ni kuombeana Baraka za mwenyezi Mungu zikae nanyi nakuwaongoza katika kila jambo.
 
Jinsi ya Kutambua Mwanamke Aliekaribu Kukuacha

Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.
 
Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo kuficha mawazo yake.
 
Back
Top Bottom