Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

54fe934549fb9020af6b19a8de3cf27f.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hivyo wengi tunaisherehekea, lakini hatufahamu asili ya sikukuu hii ambayo kwa lugha ya Kiingereza huitwa Aprils Fools.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, asili ya Siku ya Wajinga ilianza mwaka 1582 wakati ambapo Ufaransa ilibadili kalenda ya Julian na kuhamia kwenye kalenda ya Gregorian.
 
Kubadilika huku kwa kalenda kulibadilisha tarehe za mwaka na hivyo nchi hiyo ikaanza kusherehekea mwaka mpya Januari Mosi badala ya Aprili.

Lakini kwa bahati mbaya maamuzi hayo ya kubadili kalenda ya mwaka yaliyofanywa na Papa Gregory wa 13, hayakuwafikia wananchi wote wa Ufaransa na badala yake baadhi wakaendelea kusherehekea mwaka mpya Aprili Mosi. Hivyo basi waliosherehekea mwaka mpya Aprili Mosi, waliitwa wajinga na siku hiyo ikaitwa ya wajinga.
 
Vyombo vya habari, taasisi zinavyoiadhimisha siku ya wajinga

Kama ilivyo siku ya afya duniani baadhi ya taasisi kubwa duniani nazo huadhimisha Siku ya Wajinga na kuwaweka mtegoni maelfu ya watu.

Mwaka 1957 Televisheni ya Uingereza (BBC), ilionyesha kipande kifupi cha video katika kipindi cha Panorama kinachoonyesha wakulima huko Uswisi wakivuna tambi (spaghetti).
 
Dakika chache baada ya video hiyo kurushwa, mamia ya wananchi walijaa katika ofisi za shirika hilo la utangazaji wakitaka kujua aina hiyo ya kilimo cha tambi.

Mwaka 2008, BBC kwa mara nyingine walirusha video fupi iliyoonyesha pengwini(ndege mnene wa (majini asiyeweza kuruka juu)wakiruka angani na taarifa hiyo ilieleza kuwa wanyama hao wanakimbia hali ya hewa ya bara la Antarctic na kwenda America ya Kusini. Kiasili, pengwini hawezi kuruka.
 
Duka kubwa la vyakula (supermarket) la Tesco, nchini Uingereza liliweka tangazo kuwa limetengeneza karoti zinazopiga mluzi au mbinja. Tangazo hilo lilieleza kuwa karoti hizo zina nafasi katikati na ukizipika zinapiga mluzi. Wateja walimiminika kwenda kuzinunua.
 
Back
Top Bottom