Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nchini Tanzania kuna makabila mengi ambapo baina yake,kuna utani wa jadi miongoni mwao.Utani huu wa jadi upo karne na karne kabla hata nchi yetu haijawa chini ya utawala wa kikoloni,na sijui ulitokea wapi?Na kabila ambalo linaloongoza kuwa na watani wengi kutoka maeneo karibu yote nchini,ni kabila la Wasukuma na wenzao Wanyamwezi.
 
Zama hizo hadi kufikia mwanzoni wa uhuru wa Taifa letu utani wa jadi ulikuwa na nguvu.Kila mmoja alimdhihaki na kumkejeli ama kumsema hata kumcheka mtani wake mbele ya kadamnasi,kulikuwapo na vituko na majigambo yaliyofanyika ama katika ngoma za jadi na kwenye vilabu vya pombe za asili ambayo yalileta burudani ya aina yake.
 
Lakini utani huo wa jadi katika karne tulionayo,umekuwa hasi tofauti na zama za mababu na bibi zetu,sababu kubwa ikiwa ni mabadiriko ya sayansi na teknolojia.Utandawazi umekuwa athari kubwa kwa Jamii ya Watanzania kubeba asili yetu na kutawaliwa na tamaduni za kutoka nchi za Magharibi.
 
Masihara yaliofanyika yalidumisha Mila na desturi ya kila kabila la Muhusika.
Nyakati zingine;Dhihaka hizo ziliambatana na faini,hidaya na hata mchango kulingana na Nasaba moja hadi nyingine,kuwa na tukio la burudani ama huzuni,au katika mfumo wa maisha ya kila siku,
 
Mmoja kujisahau na kutenda jambo litakalotoa faida ya hidaya kwa watani zake.
Mzee wa kabila la Kingoni;Andrew Chitete {75}mkazi wa kitongoji cha Kasela Kata ya Malunga wilayani Kahama,ameonekana kutoathirika na Utandawazi uliopo kutokana na mfumo wake wa Maisha kuhakikisha anaendeleza mila na desturi hizo za Mababu na Mabibi,
 
Back
Top Bottom