Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatua hii hulipi gharama yeyote, ni bure. Baada ya kujaza fomu zao wanakupa hati na kukufungulia faili ambalo baadae ndilo huja kulitumia utakapokwenda kulipa kodi ya mapato. Ikiwa biashara yako ni ndogo sana unaweza ukaianza hivyo hivyo tu bila TIN lakini baadae ukaja kujisajili.
 
Baada ya kupata jina la biashara yako, jaribu kuuliza watu wa karibu ikiwa nao kama watalipenda. Wakiona linafaa basi lipitishe, ukiona wengi wamelitilia mashaka unaweza ukarudi tena kwenye orodha yako upya.

3. Ipe biashara yako namba ya Utambulisho wa mlipa kodi TIN
Ni vizuri ukaenda kuisajili biashara yako mamlaka ya mapato “TRA” tawi lililopo karibuni na wewe wakupe namba ya mlipa kodi (TIN).
 
4. Uchaguzi wa ni bidhaa gani utakazouza.
Kwa biashara ya duka la rejareja la mtaani hakuna ukomo wa bidhaa unazotakiwa kuuza. Cha kuzingatia hapa ni kuangalia katika utafiti wako uliofanya ni bidhaa zipi unaona wakazi wa eneo husika wanapendelea zaidi kununua.
 
Vigezo vingine ni pamoja na faida, angalia ni bidhaa zipi zenye faida kubwa kwa mfano aina fulani ya maji yanaweza kuwa yananunuliwa kwa wingi sana lakini faida yake ni kidogo mno. Hivyo ni juu yako kuamua upate faida kidogo uuze sana au faida kubwa lakini mauzo kidogo.
 
5. Andika mchanganuo wa biashara ya duka lako.
Katika vitu muhimu sana unavyopaswa kufanya kabla haujaanzisha duka lako ni kuandaa mpango kamili wa biashara, mpango unaweza kuwa upo kichwani mwako tayari lakini ni vizuri zaidi ukauandika katika karatasi hata kama hautafuata taratibu rasmi za kuandika,
 
unaweza tu ukaorodhesha mambo yako yote muhimu unayotarajia kuyafanya ili kukamilisha malengo ya biashara yako pamoja na gharama utakazotumia, pia faida au mauzo unayotarajia kwa siku, mwezi au mwaka, na tayari huo unatosha kuitwa mpango wa baishara yako.
 
Usihatarishe biashara yako uliyoilipia pango fedha nyingi na kupoteza muda wako wa thamani, hakikisha unafuata taratibu zote hasa kupata vibali kama TIN namba, leseni kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wako au manispaa na vibali vinginevyo ikiwa ni biashara kwa mfano kama ya kuuza madawa ya binadamu itabidi uende mamlaka ya chakula na dawa TFDA.
 
Amani-Ndio-Mpango-Mzima.jpg
 
Wengi wamekuwa na ndoto za kufungua maduka wakiamini yanaweza kuwa daraja la kuelekea kwenye mafanikio. Siyo mbaya kwani nawajua wengi tu ambao wamefanikiwa kwa kuanzisha vioski, baadaye maduka na sasa ni wafanyabiashara wakubwa.
 
Back
Top Bottom