Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

d56e04fbf84b5f7e301a276f401426bc.jpg
 
Ndoto za kuanzisha biashara ya rejareja hususani duka zinaweza kuwa kweli haraka na kwa urahisi zaidi endapo mtu atafuata taratibu hizi pamoja na kufanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kamili (mchanganuo) wa biashara yake iwe ni katika karatasi ama kichwani mwake.
 
Mifumo ya biashara kisheria ipo ya aina tatu;
(a) Biashara ya mtu bianafsi.
(b) Biashara ya ubia.
(c) Biashara ya kampuni yenye dhima ya ukomo (Limited company)
Biashara nyingi za rejareja hasa zile ndogo ndogo wanatumia sana mfumo huu wa biashara ya mtu mmoja au binafsi. Faida na harasa za mifumo yote 3 imefafanuliwa kwa undani sana katika vitabu mbalimbali kikiwemo kitabu kikubwa “Jifunze Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”
 
2. Chagua jina la biashara yako.
Unaweza ukawa na mpango mzuri sana wa biashara yako ya rejareja lakini ukaipa jina lisilofaa ukawa umeharibu kila kitu. Kuipa biashara jina ni hatua muhimu sana ingawa unaweza kuona ni kazi nyepesi tu kufanya hivyo. Ni kazi inayohitaji ufikirie kwa umakini mkubwa, unapotaka kuipa biashara yako ya rejareja jina linalofaa zingatia vipengele hivi hapa chini;
 
Orodhesha kwenye karatasi bidhaa ama huduma unazotoa, maneno yote yanayohusiana na biashara unayotarajia kuifanya pamoja na mazingira na eneo itakapokuwa.
· Fanya utafiti kwa kuangalia majina ya biashara kama ya kwako zilizokuzunguka, unanweza pia ukatazama kwenye mtandao wa intanet n.k mpaka utakapopata jina utakaliona unaridhika nalo.
 
Orodhesha kwenye karatasi bidhaa ama huduma unazotoa, maneno yote yanayohusiana na biashara unayotarajia kuifanya pamoja na mazingira na eneo itakapokuwa.
· Fanya utafiti kwa kuangalia majina ya biashara kama ya kwako zilizokuzunguka, unanweza pia ukatazama kwenye mtandao wa intanet n.k mpaka utakapopata jina utakaliona unaridhika nalo.
 
Jina linapaswa liwe;
ü Rahisi kueleweka kimatamshi na kimaandishi.
ü Usichague jina lenye mlengo hasi mfano mmoja ni café moja jamaa alitumia jina linalokashifu timu fulani ya mpira.
ü Usichague jina litakalopotosha watu wala lenye maana zaidi ya moja.
ü Zingatia herufi jina la biashara yako litakapoanguakia kwenye orodha kama za yellow page n.k.
 
Chagua jina litakalowakilisha kile kitu hasa utakachofanya na siyo litakalominya baadhi ya shughuli zako.
ü Chagua jina utakalojivunia na siyo litakalokufanya uone aibu hata kuliwakilisha mbela za watu.
ü Usitumie majina ya jumla yanayowakilisha vitu jumla mfano; Nafuuu store, Bei rahisi duka n.k. majina kama hayo ni vigumu kuyasajili kama alama yako ya biashara.
 
Baada ya kupata jina la biashara yako, jaribu kuuliza watu wa karibu ikiwa nao kama watalipenda. Wakiona linafaa basi lipitishe, ukiona wengi wamelitilia mashaka unaweza ukarudi tena kwenye orodha yako upya.

3. Ipe biashara yako namba ya Utambulisho wa mlipa kodi TIN
Ni vizuri ukaenda kuisajili biashara yako mamlaka ya mapato “TRA” tawi lililopo karibuni na wewe wakupe namba ya mlipa kodi (TIN).
 
Back
Top Bottom