Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yasome vizuri mazingira ya kazi yako na kufuata mdundo
Kila ofisi ina mazingira yake na namna inavyojiendesha. Ili usiingie katika msongo wa mawazo anza kuyasoma mazingira ya kazi yako kwa umakini mkubwa kwa kufuatilia mikataba yako, kuwafahamu vizuri maboss na walio chini yako kitabia na namna wanavyofanya kazi.
 
Mfahamu kila mmoja unaefanya nae kazi ili umtengenezee picha ya namna ya kuishi naye vizuri. Hii itakusaidia kuepuka kushtukizwa kwa maamuzi usiyoyategemea au kauli usizotegemea kutoka kwa mtu husika. Unapoona mambo yanakuwa magumu, ishi kwa mujibu wa mazingira husika ya kazi. Yaani fuata mdundo wa muziki unaopigwa lakini kuwa muangalifu sana usiingie kwenye mtego.
 
Timiza majukumu yako kwa ufanisi na kwa wakati, wasiliana kwa kujiamini
Jitahidi kutimiza majukumu yako kwa muda na kwa wakati ili kuepusha kutokubalika kazini kwa kuchelewesha mambo. Unaweza kuhisi unasumbuliwa na boss wako, kumbe wewe ni chanzo cha usumbufu huo.
 
Jiamini
Amini kuwa wewe ndiye unayefaa kufanya kazi husika, amini ofisi uliyopo hukuipata kwa kubahatisha hivyo ufanisi wa kazi zako na CV yako ndivyo vinavyokubeba. Hii itakufanya kufanya kazi yako kwa kujiamini (lakini usipitilize). Usiamini kuwa kazi hiyo ndiyo iliyobeba maisha yako yote
 
bali amini ndiyo iliyobeba stamina ya uchumi wako kwa wakati huo na unaihitaji sana. Hii itakufanya kufanya kazi kwa bidii kupata unachotaka ili upige hatua kimaisha kuliko kufikiria kuwa hakuna maisha nje ya hiyo kazi. Hivyo, hii itakufanya kuwajibika zaidi na kuitunza ‘mood’ yako pale unapovurugwa.
 
Sikiliza, Tafakari, Uliza, Tekeleza
Ili ukwepe msongo wa mawazo na kupenda mazingira ya kazi yako, unapaswa kumsikiliza kwa makini mteja au mtu yoyote anayezungumza na wewe mambo ya kazi. Sikio lako lisibague usikivu kwa kuangalia anayeongea ni nani.
 
Kiukweli! I'm not comfortable na wale wanaoandika manamba tu kama manamba wa mashamba ya mkonge kule tanga..T413....T716....its boring!

Writes something educative and informative. Tuelimike hata kidogo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
I understand you totally. Tuvumiliane tu hivyo hivyo. Pamoja na kuburudika, wengine tupo hapa kujifunza funza vitu na kujenga urafiki; na hata kupeana mbinu za ujasiriamali. Wengine wapo hapa solely kwa sababu ya likes. Na kuweka namba ni rahisi zaidi kuliko sisi kuhangaika ku-type kuendeleza maongezi na utani. Tuvumiliane tu hivyo hivyo mkuu.
 
Kila linalozungumzwa kuhusu kazi ni muhimu sana kwani ukiteleza kupitia hilo litakuletea matatizo ambayo yanaweza kuanza kidogo na kulipuka kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa kuhisi unasakamwa ofisini.
 
Back
Top Bottom