Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kashata za maziwa mazito (condensed milk. 1. vikopo 2 maziwa mazito sona 2.kikombe 1 cha chai sukari 3.nazi fresh ilokunwa vikombe chai 2 4.ufuta ulokwisha kaanga nusu kikombe 5.blue band vijiko vya mezani 2 6.vanila vijiko vya chai 2 *Changanya vitu vyote uweke kwenye sufuria isipokua Ufuta na Nazi.hivi unaweka mwisho wakati mchanganyiko wako unapoanza kuwa mzito wakati unakoroga. Ukishachanganya vitu nilokutajia koroga taratibu ukiwa unatumia Moto mdogo. Koroga mpaka mchanganyiko unakuwa mzito ndio weka Ufuta na Nazi.endelea kukoroga mpaka Rangi inapobadilika kuwa brown. Paka sinia mafuta kisha mwagia mchanganyiko wako.weka upoe kisha kata shepu utakayo. Yaani hizi Hazina tofauti na tofi. Enjoy -
 
Maandazi sidhani kama kuna mtu hayapendi.lugha nyingine watu huita Mahamri. Kipimo nilichotumia ni hiki. .Kg 1 unga Wa Bakhresa PPF .Hamira kijiko cha mezani 1 (tbspn) .Baking powder robo kijiko cha Chai.hata ile iloandikwa chapa mandashi in sawa. .Mafuta mepesi vijiko Vya mezani 5 .Sukari weka kikombe kimoja cha Chai usijaze sana.ninavyosema kikombe cha Chai no kila cha kawaida huja na kisahani chake.sio mug. Weka hiliki ilosagwa kijiko 1 cha Chai.ukipenda weka vanilla nusu kijiko.angalia vanilla ukizidisha huleta uchungu.
 
Namna ya kufanya. Chukua unga chekecha,weka kwenye bakuli,tia sukari,hamira,baking powder,hiliki changanya vizuri.kisha weka Mafuta pikicha vizuri,weka Maji glasi 1 ya kawaida ulotia vanilla ndani.anza Maji weka kati ya unga kidogo kidogo,ule unga unaopata Maji weka pembeni.kisha ukande wote kwa pamoja,kama Maji yatapungua ongeza kidogo.unga usiwe mgumu na usiwe mtepe uwe Wa kawaida. Kata madonge 5 weka duara nzuri.kisha sukuma usiwe mwembamba mduara wako.halafu kata Mara 4 .ina maana ukimaliza hapo utakuwa na maandazi 20. Weka sinia nyunyizia unga panga Mandazi na ngoja yaumuke yavimbe.ukitaka kujua kama andazi limeumuka,libebe,kama jepesi basi litakuwa tayari kuchomwa.na kama ni zito basi subiri liumuke. Unapotenga karai La Mafuta kabla hujatia andazi,kwanza tupia kipande kidogo cha andazi kuona kama Mafuta yapo tayari kuchoma maandazi yako.Mafuta yakiwa ya moto sana maandazi usiyaweke ujue yatatoa vipelevipele.ukiweka Mafuta kama hayajachemka ujue maandazi yako yatanyonya Mafuta.yawe ya moto Wa kawaida.
 
Vitu vinavyo Fanya Nyama iwe laini katoka kuiunga. 1.Tangawizi fresh 2.papai bichi 3.majani ya chai 4.mtindi. 5.tunda liitwalo kiwi. Sina maana uvitie vyote kwa pamoja.hii nimekupa mfano ukiwa utakosa hiki weka kile. Utakacho chagua hapo hakikisha umesaga na ndio uweke kwenye mchanganyiko wa Nyama yako. Nyama haitaki makorokoro kuipata ladha yake. -
 
Vitunguu vina faida nyingi. Leo tutazungumzia vitunguu licha ya kuwa kiungo kizuri kwenye Chakula,vitunguu kinga Kubwa kwenye Chakula chako ikiwa kwa bahati mbaya umezidisha chumvi kwenye Chakula,basi chukua kitunguu kimoja kikubwa menya na weka ndani ya Chakula kilozidi chumvi.basi utastaajabu hicho vitunguu kitakavyo nyonya hiyo chumvi. -
 
GINGER CARDAMOM MILK TEA / CHAI YA MAZIWA YA TANGAWIZI NA ILIKI : Mahitaji: Maziwa vikombe 3 Majani ya chai 1/2 kjk cha kula Sukari kiasi Tangawizi iliyotwangwa 1/2 cha chai Hiliki punje 5-6 Maji kikombe 1 Maelekezo: Menya maganda ya tangawizi na twanga tangawizi na hiliki Chemsha maziwa na maji yakianza kuchemka tia majani ya chai, tangawizi na hiliki ilotwangwa. Weka moto wa kati na acha chai iwive na kuwa na rangi nzuri na harufu nzuri. Zima jiko kisha chuja chai yako tia sukari na ukoroge. Chai tayari kwa kunywa.enjoy
 
MOROCCAN BREAD ( BATBOUT ) / MIKATE YA MOROCCO ( BATBUT ) : Mahitaji : Unga Hamira Maziwa ya unga Sukari Chumvi Mafuta Kuhusu vipimo inategemea wingi wafamilia yako,kwamfano mm nilipika : Vikombe 3 vya unga wa ngano Hamira kjk cha kulia 1 Maziwa ya unga kjk cha kulia 1 Sukar kijiko cha kulia 1 Chumvi kijiko cha chai 1 Mafuta kiasi Jinsi ya kupika : Changanya vitu vyote kwenye unga.. kisha tia maji kiasi uchanganye unga kama vile unachanganya unga wachapati, kisha kata madonge yaache yaumuke kidogo kisha yasukume kama ya chapati lkn haya uyafanye yawe manene kidogo. Kisha anza kuyapika uyaache yavimbe Yakitokea brown yanapendeza zaidi. ( UNAZIPIKA BILA YA MAFUTA HAZIKAANGWI NA MAFUTA.. CHOMA KWENYE CHUMA CHA CHAPATI BILA YA KUWEKA MAFUTA ZINAIVA BILA YA MAFUTA ) Hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa,enjoy
 
Leo tunaangalia namna nyingine ya kuandaa tambi. Pishi hili maarufu kama Sphagetti bolognese,ni mchanganyiko wa tambi,nyama ya kusaga na njegere(optional). MAHITAJI: 1. Tambi mfuko mmoja 2. Nyama ya kusaga nusu kilo 3. Nyanya 4 4. Kitunguu swaumu 1 5. Kitunguu maji kikubwa 1 6. Njegere glass ndogo 1 7. Karoti 1 na Hoho 1 8. Chumvi kiasi JINSI YA KUANDAA: -Weka mafuta yachemke,kisha kaanga kitunguu swaumu kilichopondwa pamoja na kitunguu maji,hoho na karoti. -Weka nyama katika mchanganyo huo na ikaange hadi itakapobadilika rangi kuwa ya brown. -Weka tambi zilizochemshwa na njegere. -Koroga kisha ongeza nyanya(ni vizuri zikawa zimesagwa kuliko kukatwakatwa) kisha ongeza maji kidogo. -Funika acha ichemke,kisha weka chumvi. -tayar kwa kuliwa, inaweza kuliwa kama chakula cha wakati wowote,pamoja na kinywaji chochote. Enjoy -
 
TAMBI ZA DENGU Mahitaji : Unga wa dengu kilo 1 Chumvi kiasi Pilipili manga kiasi Pilipili ya unga kiasi Manjano kijiko 1 cha chai Baking soda 1/2 kijiko cha chai Mafuta ya kula kikombe 1 Maji vugu vugu kiasi cha kukandia NAMNA YA KUTAYARISHA: 1. Changanya vitu vikavu vyote vizuri katika bakuli, tia mafuta kisha changanya tena ufanye chenga. 2. Anza kutia maji taratibu hadi upate unga mlaini, paka mikono yako mafuta kisha kanda unga kwa muda wa dk 5 3. Funika na uache ukae kwa muda muda wa dk 10. Bandika mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi 4. Utie unga wako katika mashine ya tambi kisha binya taratibu kuruhusu tambi kutoka na kudondoka kama mvua katika mafuta ya moto kisha taratibu zungusha mzunguko mmoja na acha ziive na kupata rangi pande zote mbili (angalia picha katika comments) 5. Epua katika chujio zichuje mafuta, rudia utaratibu kwa unga wote. Taratibu zivunje vunje na tambi zako zitakuwa tayari kwa kula. Enjoy!
 
Upishi wa pilau la viungo visivyosagwa lenye taste haswa,wengi tunapika pilau zinakosa taste, fuatisha maelekezo haya,utapata matokeo chanya... Mahitaji: Mdalasini Binzari nyembamba Iriki Karafuu Pilipili manga Giligilani Vitunguu swaumu +tangawizi twanga pamoja Mafuta,chumvi,mchele nyama (uipendayo) Viazi mviringo Vitunguu maji UANDAZI Chemsha nyama isiive sana iwe na ugumu kdg,achia supu nyingi kiasi cha kuivishia mchele wako Weka sufuria jikoni tia mafuta yakilata moto weka kitunguu maji,kaanga mpaka kiwe brown,weka viazi kaanga kidg weka nyama bila ile supu,kaanga kdg,weka maji ya kawaida kdg sana,then weka mchanganyiko wa swaumu na tangawizi, endelea kukoroga,then weka viungo vyotr kasoro binzari nyembamba Then kaanga kdg weka mchele na chumvi, acha dk 5 hk ukiwa umefunika Then weka ile supu yako nyunyuzia binzari nyembamba juu Funika mvuke usitoke mpk chakula kitapokauka, palipila km unatumia mkaa au weka kwenye oven Then kikishakuwa tayari pakua kwa kuliwa na kachumbari, KARIBUNI....
 
Jinsi ya kuondoa weusi na harufu mbaya ya kikwapa Mahitaji Limao limoja Baking soda kijiko cha chai Chumvi kiasi Njia Safisha kikwapa kisha kikaushe kiwe kikavu Kisha changanya limao bakingsoda na chumvi na paka haraka kwenye kikwapa Acha kwa muda wa dakika 15 na kisha osha kikwapa chako Hii unaweza fanya mara 3 kwa wiki kwa matokeo bora zaidi na chamsingi zingatia usafi kuepusha kikwapa kutoa harufu na na kuwa cheusi na pia aina ya vipodozi unavyopaka kwenye vikwapa -
 
Muda sahihi wa kunywa maji 7:00 glasi ya 1 Kunywa kikombe cha kwanza cha maji baada ya kuamka husaidia mambo mengi sana na pia hurudisha maji yaliyopotea wakati umelala na kunywa chai angalau baada ya nusu saa baada ya kunywa maji 9:00 glasi ya 2 Baada ya lisaa limoja kupita baada ya kunywa chai ya asubuhi kunywa glasi ya maji ili kuanza siku 11:00 glasi ya 3 Pata glasi ya maji nusu saa kabla ya kupata chakula cha mchana 13:30 glasi ya 4 Kunywa glasi ya maji lisaa baada ya kupata chakula cha mchana ili kuruhusu virutubisho kutoka kwy chakula kufonzwa na mwili 15:00 glasi ya 5 Pata glasi ya maji kutokana na kupoteza maji na shughuli mbalimbali 17:00 glasi ya 6 Kunywa glasi nyingine ta maji ili kukusaidia kutokula chakula kingi cha jioni (dinner) 20:00 glasi ya 7 Pata glasi ya maji lisaa limoja baada ya chakula cha jioni (dinner ) na kabla ya kuoga 22:00 glasi ya 8 Kunywa glasi ya maji lisaa kabla ya kulala hii husaidi kutengeneza seli wakati umelala NB:Muda mzuri wa kunywa maji ni baada ya kuamka,kabla na baada ya kupata chakula,kabla ya kuoga na kabla ya kulala -
 
Faida za maji ya uvuguvugu na limao asubuhi kabla ya kupiga mswaki 1. Husaidia kupunguza uzito 2.Husaidi mfumo wa usagaji wa chakula 3.Husaidia kuongeza nguvu ya maini na kusafisha maini kwa kutoa taka mwili 4.Husaidia kupigana na magonjwa 5.Husaidia kungarisha ngozi Mahitaji Maji ya uvuguvugu glass 1 Malimao 2 Njia Chukuwa maji ya uvuguvugu na kamulia malimao na unywe asubuhi ukiamka kabla ya kupiga mswaki
 
DONDOO ZA AFYA BORA 1. mazoezi. Kwa siku jaribu kupata hata dakika 30 za kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya na mwili kwa ujumla unaweza kutembea,kukimbia,kuogelea,kuendesha baiskeli nk 2.chakula bora. Tunitahidi sana kupunguza kula vyakula vyenye wanga,mafuta na vyakula vilivyosindikwa na kujitahidi kula kwa wingi matunda,maji,mbogamboga za majani,samaki na mbegu mbegu kama karanga,ufuta 3.kupunguza uzito. Ukiwa na na uzito mkubwa ni hatari kwa afya na hii inatokana na kula vyakula vyenye calories nyingi husababisha mwili kushindwa kuunguza so kula kidogo inasaidia na inasaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa kama moyo,kisukari nk
 
DONDOO ZA AFYA BORA 1. mazoezi. Kwa siku jaribu kupata hata dakika 30 za kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya na mwili kwa ujumla unaweza kutembea,kukimbia,kuogelea,kuendesha baiskeli nk 2.chakula bora. Tunitahidi sana kupunguza kula vyakula vyenye wanga,mafuta na vyakula vilivyosindikwa na kujitahidi kula kwa wingi matunda,maji,mbogamboga za majani,samaki na mbegu mbegu kama karanga,ufuta 3.kupunguza uzito. Ukiwa na na uzito mkubwa ni hatari kwa afya na hii inatokana na kula vyakula vyenye calories nyingi husababisha mwili kushindwa kuunguza so kula kidogo inasaidia na inasaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa kama moyo,kisukari nk
 
4.kupima. Ni vizuri tuwe na tabia ya kufanya vipimo hospital hata mara moja kwa miezi 4 ili kupata kujua afya zetu na magonjwa ambayo ukiwahi yanaweza kutibika kiurahisi mfano kansa ya maziwa kwa akina mama,sukari nk hasa watu wenye miaka 50 na zaidi wanatakiwa kuzingatia hili sana. 5.kuepuka mawazo. Ni vizuri kujiwekea mipaka katika maisha na kuhakikisha unajitahidi kuepuka mawazo ambayo yatakuletea madhara na kujitahidi kuchanganyika na familia na marafiki,kufanya mazoezi,kupata muda mzuri wa kulala .
 
Back
Top Bottom